Viongozi wa Afrika wakutana kujadili mageuzi katika Umoja wa Afrika


Rais wa Rwanda Paul Kagame amewahimiza viongozi wenzake wa nchi za Afrika kufikia makubaliano kuhusu maguezi yaliyojadiliwa kwa muda mrefu kuhusu Umoja wa Afrika. Kagame ameyasema hayo katika mkutano maalumu wa kilele wa Umoja huo unaofanyika Addis Ababa, Ethiopia.

Je, mageuzi yatafikiwa?

Viongozi wa nchi na mawaziri kutoka nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika wanakutana katika makao makuu ya Umoja huo katika kile kinachoonekana juhudi za dakika ya mwisho za kufikia makubaliano kuhusu haja ya kuufanyia Umoja wa Afrika mageuzi, mazungumzo ambayo yamedumu kwa takriban miaka miwili.

Ruanda Kigali Unterzeichnung Afrikanisches Freihandelsabkommen (Imago/Xinhua/G. Dusabe)

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Kagame ambaye ni mwenyekiti wa Umoja huo amesema kuna haja ya dharura ya kutekeleza maguezi katika umoja huo ambao mara nyingi unaonekana kutokuwa na nguvu na unaotegemea pakubwa misaada kutoka kwa wafadhili.

Akiufungua mkutano huo maalumu wa kilele, Rais huyo wa Rwanda amesema matukio barani Afrika na kwingineko duniani yanathibitisha umuhimu na haja ya dharura ya kutekeleza mabadiliko kwa lengo la kuifanya Afrika imara zaidi na kuwapa watu wake mustakabali unaostahili wa siku za usoni.

Muhula wa Kagame wa kuhudumu kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika unakamilika mwezi Januari na wachambuzi wanasema muda unayoyoma kwa kiongozi huyo kutekeleza mpango wake wa kuleta mageuzi katika umoja huo huku Misri ikitarajiwa kuchukua uenyekiti huo mwaka ujao na ikiwa haina urari wa kuendeleza ndoto hiyo ya kuleta mageuzi.

Kwenye mapendekezo yaliyozinduliwa mwaka jana, Kagame alinuia kufikia halmashauri yenye mamlaka zaidi iliyo na maafisa wachache ambayo gharama zake zitagharamiwa na nchi wanachama badala ya wafadhili wa nchi za kigeni. Lakini nchi kubwa za Afrika zina mashaka na halmashauri yenye nguvu kubwa inazoamini itaingilia uhuru wa nchi hizo za kujitawala zinavyotaka.

Kiongozi wa Ethiopia asifiwa

Kagame alipendekeza pia nchi wanachama wamchague mwenyekiti wa halmashauri ya Umoja wa Afrika ambaye atakuwa na mamlaka ya kumteua naibu wake na makamishna wa halmashauri hiyo, pendekezo ambalo lilikataliwa na viongozi.

Äthiopien Abiy Ahmed Premierminister (picture-alliance/AP Photo/Saudi Press Agency)

Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed

Pia alitaka kupunguza majukumu ya Umoja wa Afrika kutuama katika nyanja nne ambazo ni amani na usalama, utangamano wa kiuchumi, masuala ya kisiasa na uwakilishi wa Afrika katika safu ya kimataifa.

Viongozi wa Afrika wamemsifu waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwa kuleta mageuzi makubwa nchini mwake.

Abiy mwenye umri wa miaka 42 amewaeleza viongozi wa Afrika wanaokutana katika mkutano maalumu wa kilele kuhusu Umoja wa Afrika kuhusu mageuzi aliyoyafanya tangu alipoingia madarakani mwezi Aprili mwaka huu.

Miongoni mwa mageuzi hayo ni kuwaachia huru maelfu ya wafungwa, kuviondolea marufuku vyama vya kisiasa, mashirika ya habari na mitandao, kuleta maridhiano na kupambana na ufisadi.

Waziri huyo mkuu wa Ethiopia amewahimiza viongozi wengine wa Afrika kufanya mageuzi makubwa ili kupiga hatua katika amani na maendeleo barani Afrika.

Mwandishi: Caro Robi/AFP/AP

Mhariri: Lilian MtonoSource link

Jamal Khashoggi: CIA 'yamlaumu mwanamfalme wa Saudia '


mwanamfalme Mohammed bin Salman

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Saudi Arabia inasema mwanamfalme Mohammed bin Salman hakuhusika na mauaji ya Khashoggi

Shirika la ujasusi la Marekani(CIA) linaamini kuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman wa Saudi Arabia ndiye aliyeamuru kuuawa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi.

Vyanzo kutoka shirika hilo vinasema kuwa vina ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa huenda mrithi huyo wa ufalme wa Saudi Arabia alijuwa kuhusu mipango ya kumuua Khashoggi.

Kauli hiyo ya CIA, iliyoripotiwa kwanza na gazeti la Washington ni ya hali ya juu kabisa kutolewa na Marekani mpaka sasa, ikimuhusisha moja kwa moja mtawala huyo mtarajiwa wa Saudi Arabia na mauaji hayo.

Ikulu ya Marekani na Wizara ya Mambo ya nje hazijasema lolote kuhusiana na suala juu hilo.

Msemaji wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington amesema tathmini hiyo ni ya uongo.

“Tumekuwa na tukituhumiwa kwa madai mbalimbali na mpaka sasa hatujabaini lolote la msingi kuhusu madai hayo,”

Haki miliki ya picha
EPA

Siku ya Ijumaa (Novemba 17), Mwanamfalme Khaled aliandika kwenye mtandao wa Twitter kwamba mawasiliano yake ya mwisho na Khashoggi yalikuwa kupitia ujumbe wa maandishi ya simu ya mkononi tarehe 26 Oktoba 2017, takribani mwaka mmoja kabla ya kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Huku hayo yakijiri ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini Saudi Arabia imemaliza uchunguzi wake juu ya nani aliyeamuru kuuawa kwa mwanahabari Jamal Khashoggi.

Uchunguzi huo umebaini kuwa mauaji hayo yaliamuriwa na afisa mwandawizi wa idara ya usalama wa taifa ya Saudia ambaye alipewa kazi ya kumshawishi Khashoggi kurejea Saudia.

Mwanahabari huyo ambaye alikuwa kinara wa kumkosoa Bin Salman alikimbia Saudia mwaka 2017 na kuhamia Marekani.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi hiyo, Khashoggi alidungwa sindano ya sumu baada ya purukushani kuibuka ndani ya ofisi ndogo za ubalozi wa nchi hiyo jijini Istanbul, Oktoba 2, 2018.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Watu wakishiriki ibada ya wafu ya mwanahabari Jamal Khashoggi

Tayari ibada ya wafu imefanyika nchini Saudi Arabia na Uturuki

Salah,Mwana wa kiume wa Khashoggi, aliungana na mamia ya waombolezaji waliyohudhuria ibada mjini Jeddah huku mamia ya waombolezaji wengine wakifanya ibada hiyo ya maombi katika miji mitakatifu ya Mecca na Medina.

Watu 11 tayari wameshafunguliwa mashtaka kutokana na mkasa huo na waendesha mashtaka wanataka watano kati yao kupatiwa adhabu ya kifo.

Uchunguzi unaendelea kwa watu wengine 10 ambao wanshukiwa kushiriki mauaji hayo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Salah, mwana wa kiume wa Khashoggi akiwakaribisha waombolezaji katika mji wa Jeddah sik ya Ijumaa

Katika mkutano na waandishi wa habari, Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Saudia Shalaan bin Rajih Shalaan amesema mwili wa Khashoggi ulikatwa katwa ndani ya ubalozi baada ya kuuawa.

Vipande hivyo vya mwili vilikabidhiwa kwa mshirika wao ambaye ni raia wa Uturuki nje ya ubalozi.

Tayari picha ya kuchora ya mshirika huyo imetolewa na uchunguzi unaendelea kujua vipande hivyo vya mwili vilipelekwa wapi.

Bwana Shalaan hata hivyo hakuwataja wale ambao wamefunguliwa mashtaka juu ya tukio hilo.Source link

Serikali yakamata tani 20 za korosho katika ghala binafsiWaziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema Jumamosi kuwa korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu, limeripoti gazeti la Mtanzania.

“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.

Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje ya nchi au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hicho, Jumanne wiki hii, tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.

Pia imeripotiwa kuwa siku ya Alhamisi iliyopita yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yalioingizwa kutoka Msumbiji.Source link

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Pulisic, Hysaj, Fabinho, Origi, Rodriguez, Dembele


Christian Pulisic

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Christian Pulisic,winga wa Borussia Dortmund

Chelsea inajiandaa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Christian Pulisic,20,- Wanapania kukamilisha usajili huo kufikia Januari. (Mail)

Beki wa Napoli Elseid Hysaj, 24, huenda pia analengwa na Chelsea, kwa mujibu wa ajenti wake. (Radio CRC, via Sun)

Juventus imeungana na AC Milan kuonyesha azma ya kumnunua kiungo wa kati wa Liverpool Fabinho 25. (Sport Mediaset, via Talksport)

Winga wa Real Madrid Mcolombia James Rodriguez huenda akajiunga na ligi ya Primia msimu ujao wa joto.

Barcelona imesisitiza kuwa haina mpango wa kumuuza winga wake Ousmane Dembele, na kwamba haijapata ofa yoyote kumhusu. (Cadena Ser, via Evening Standard)

Nahodha wa Manchester United Antonio Valencia, 33, anadai kuwa meneja wake Jose Mourinho amemtema kama nahodha wake na kwamba hana jeraha lololote. (Area Deportiva, via Mail)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Antonio Valencia

Galatasaray inataka kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi kwa mkopo mwezi Januari. (ESPN)

Wolves anataka kumpatia Origi mkataba wa kudumu, na tayari wameweka dau la euro milioni 20. (Mirror)

Mlinzi wa Arsenal Julio Pleguezuelo, 21, amesema kuwa amepokea ofa kadhaa za kurejea Uhispania lakini anataka kuendelea kusalia Emirates. (Marca – in Spanish)

Tottenham wameonywa kuwa uwanja wao mpya huenda usiwe tayari kutumika hadi mwezi Machi kutokana na changamoto za hapa na pale katika eneo la ujenzi. (Times)

Haki miliki ya picha
EPA

Kiungo wa kati wa Liverpool na England Alex Oxlade-Chamberlain, 25, anapania kurujea uwanjani baada ya kuumia goti mwishi wa msimu uliyopita. (BetVictor, via Liverpool Echo)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani ameahidi kuwapeleka wachezaji wake Las Vegas ikiwa watafaulu kupanda daraja na kujiunga na ligi ya Primia.(Mail)

Meneja mpya wa Fulham Claudio Ranieri amewafurahisha wakubwa wake wakati wa mahojiano ya kazi baada ya kuwaelezea kinaga ubaga kwa nini timu hiyo haifanyi vizuri na ni wapi panastahili kufanyiwa ukarabati. (Mail)

Bora ya Ijumaa

Teknolojia ya VAR au ya kutumia video kutoa uamuzi itaanza kutumika katika ligi kuu ya England msimu ujao baada ya vilabu vinavoshiriki ligi hiyo kukubaliana kimsingi.

Tayari majaribio yamekuwa yakifanywa katika baadhi ya mechi za msimu huu.

Wasimamizi wa mechi za ligi hiyo wanatarajiwa kutuma ombi rasmi kwa bodi ya kimataifa ya kandanda na shirikisho la kandanda duniani FIFA.

Haki miliki ya picha
BBC Sport

Klabu ya Chelsea huenda ikafungiwa kufanya usajili kwa miaka miwili ikiwa itapatikana na hatia ya kukiuka kanuni za usajili.

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limekuwa likiwachunguza The Blues kwa miaka mitatu.

Uchunguzi huu ni kuhusu kusaini wachezaji waliyo chini ya miaka 18, ikiwa ni pamoja na mchezaji wa zamani Bertrand Traoré(Football leaks)

Arsenal inamfuatilia beki wa kati wa Sebastian Walukiewicz,18 ambaye anachezea klabu ya Pogon Szczecininayoshiriki ligi ya Poland.

Gunners hata hivyo inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa miamba wa La Liga Barcelona. (Football London)Source link