Almasi la waridi kutoka Afrika kusini yavunja rekodi ya thamani duniani


Pink Legacy diamond

Haki miliki ya picha
AFP/Getty

Image caption

Mmiliki mpya wa almasi ya rangi ya waridi imebadilishwa jina na kuitwa ‘Winston Pink Legacy’

Almasi yenye rangi ya waridi huwa ni adimu kupatikana na gharimu yake ni dola milioni 50 kwa karati.

Almasi hiyo ambayo ni ghali na ina uzito wa chini ya karati 19.

Almasi la waridi ilinunuliwa na chapa ya Harry Winston mwenye asili ya Marekani katika mnada uliofanyika Geneva.

“Karati moja inagharimu takribani dola milioni 2.6 na bei hiyo inathibitisha kuwa almasi ya rangi ya waridi ina gharama kubwa zaidi duniani”, kwa mujibu wa mkuu wa nyumba ya mnada barani ulaya, Christie.

Almasi hiyo inayokadiriwa kuwa na thamani ya kati ya dola milioni 30 mpaka dola milioni 50 baada ya kuuzwa kwenye mnada ndani ya dakika tano.

Haki miliki ya picha
AFP/Getty

Image caption

Almasi hiyo iliuzwa kwa muda wa dakika tano

Mmiliki mpya wa almasi ya waridi ameipa jina la Winston Pink Legacy.

“Mwanzoni almasi hiyo ilikuwa inamilikiwa na familia ya Oppenheimer ambayo ilikuwa inamiliki mgodi wa De Beers,

Unaweza kusema kwamba almasi yenye rangi ya waridi ina uzito wa karibu karati 19 .

Hii inashangaza,” Rahul Kadakia kutoka duka la kimataifa la vito alieleza.

Na almasi hii inadaiwa kuwa ni ya kifahari na iko katika daraja la juu zaidi ya almasi nyingine.

Kipande hicho kilipatikana katika mgodi mmoja wa Afrika kusini takribani miaka mia moja iliyopita na inawezekana hakikuwahi kubadilika tangu mara ya kwanza ikatwe mwaka 1920,

Christe alibainisha.

Almasi ya kifahari ya waridi ambayo ina uzito mkubwa zaidi ya karati 10 iliuzwa katika mnada wa almasi ya waridi iliuzwa kwa duka la kimataifa vito.

Mwezi Novemba 2017,8.14 karati ya rangi ya waridi iliuzwa kwa dola 17,768,041 mjini Hong Kong na karati nyingine ziliuzwa dola milioni 2.1kwa karati.Source link

Siku ya Kupambana na Kisukari Duniani


Kipindi cha muda miwili kimetolewa kuwa bora katika kufikia kampeni ya Siku ya Kisukari Duniani, kuhusu mpango wa kimkakati wa Shirikisho la Kimataifa la Kisukari na kuwezesha kupanga, kuendeleza, kukuza na kushiriki.

Vifaa na hatua zitakazohukuliwa na shirikisho hilo katika muda huo wa miaka miwili ya kampeni dhidi ya kisukari inapania kutoa hamasisho kuhusu athari ya kisukari kwa familia na mfumo wa kuwasaidia walioathirika. Kadhalika kuzisaidia familia katika juhudi za kukabili, kuwahudumia, kuzuia na kuelimisha kuhusu kisukari.

Zaidi ya watu milioni 425 wameathirika na kisukari. Visa vingi vya ugonjwa huo ni vya daraja ya pili, ambayo inaweza kuzuiwa kupitia mazoezi ya kila siku, vyakula vyenye afya, na kuishi katika mazingira bora. Familia zina jukumu kuu katika kushughulikia mambo yanayichangia kisukari hiyo ya daraja la pili, na lazima wapewe mafunzo, raslimali na mazingira ya kuishi maisha mazuri.

Mtu mmoja kati ya wawili wanaoishi na kisukari bila kutambuliwa. Kugunduliwa mapema na kupata matibabu ni muhimu katika kuzuia matatizo yanayochangiwa na ugonjwa wa kisukari, hivyo uhamasisho kuhusu ishara, dalili, na mambo hatari kuhusu aina zote za kisukari ni muhimu sana ili kusaidia kuugundua mapema.

Symbolbild - Insulin: Hilfspfleger unter Mordverdacht (picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd)

Sindano ya Insulini

Ugonjwa wa kisukari unaweza kuwa wa gharama kwa mtu au familia. Katika mataifa mengi, gharama ya sindano ya insulini na ufuatiliaji pekee unaweza kutumia nusu ya mapato familia, na wengi wanashindwa kupata dawa za kisukari mara kwa mara na huduma. Shirikisho la Kimataifa la Kisukari linasema hali hiyo inaashiria kuwa ni lazima kuzuia gharama kuongezwa kwa waathirika na familia zao, suala ambalo linaathiri matokeo ya afya.

Shirikisho hilo linasema kuwa ni mtu mmoja miongoni mwa watu wanne wa familia moja anaweza kufikia mipango ya elimu kuhusu kisukari. Usaidizi wa familia katika kuwahudumia waathiriwa wa kisukari umetajwa kuboresha matokeo ya afya kwa waathiriwa hao.

Kutokana na hilo Shirikisho la Kimataifa la Kisukari limesema ni muhimu kwa elimu inayoendelea kutolewa kuhusu kukabili kisukari kupatikana kwa urahisi kwa waathiriwa pamoja na familia zao, ili kupunguza athari za kihisia ambayo inaweza kuathiri ubora wa maisha.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/ www.worlddiabetesday.org

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

 Source link

Utafiti umebaini kuwa wazazi hawana ufahamu kuhusu uwezekano wa watoto wao kuugua ugonjwa wa kisukari.


Mwanamke wa kisomali akimshikilia mtoto wake anayeugua kisukari Kaskazini Mashariki mwa Kenya

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mwanamke wa kisomali akimshikilia mtoto wake anayeugua kisukari Kaskazini Mashariki mwa Kenya

Ulimwengu unapoadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari, utafiti uliyofanywa na shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari (IDF) umebaini kuwa wanne kati ya wazazi watano hawana uwezo kung’amua dalili za mapema za ugonjwa huo kwa watoto wao.

Awali ugonjwa wa kisukari ulihusishwa na watu wanene na wazee lakini miaka ya hivi karibuni watoto wachanga pia wamejikuta wakikabiliwa na maradhi hayo.

Ili kufahamu kwanini watoto pia wanakabiliwa na ugonjwa huu BBC imezungumza na Farhia Mohammed kutoka mtaa wa Eastleigh jijini Nairobi, anayemuuguza mtoto wake wa miaka minane ambaye alipatikana na ugojwa wa kisukari akiwa mdogo.

Farhia anasema hana budi kumpikia chakula maalum mwanawe ili aweze kudhibiti kiwango cha sukari mwilini mwake.

”Nikiamka nafikiria kile kitu nitampatia, lazima iwe chakula asili, kama anaenda shule lazima apate mlo kamili”

Mtoto huyo aligunduliwa kuwa anaugua kisukari alipokuwa na miaka minne. Mama Farhia anasema hakuwa na ufahamu mwanawe anaugua kisukari

”Niliona mtoto anaenda msalani mara kwa mara hali ambayo nilihisi si ya kawaida”

Anasema alipompeleka hospitali hawakuruhusiwa kurudi nyumbani kwa sababu mtoto alihitajika kupewa matibabu ya dharura.

Haki miliki ya picha
Reuters

Lakini swali ni je ni kwanini watoto wanapatikana na maradhi ya kisukari wakiwa wadogo?

Abdisalan Mohammed ambaye ni daktari wa watoto anasema ugonjwa wa kisukari umekuwepo tangu zamani.

Anaongeza kuwa tofauti na miaka ya nyuma siku hizi kuna maabara ambayo wataalamu wanatumia kufanya utafiti ilikubaini ikiwa mtoto ana ugojwa huo.

Dkt Abdisalan anasema”kwa kweli 10% ya ugonjwa wa kisukari unapatikana kwa watoto wachanga kwa hivyo watu wasifikirie kuwa huu ni ugonjwa wa watu wazima pekee”

Watoto hususan hupatikana na aina ya kwanza ya kisukari ambayo inahitaji mgonjwa kudungwa dawa ya insulin ili kudhibiti kiwango cha sukari mwilini.

Kisukari ni ugonjwa gani?

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2017 ya shirikisho la kimataifa la ugonjwa wa kisukari karibu watu milioni 15.5 waliyo na umri kati ya miaka 20-79 wanaishi na ugonjwa huo barani Afrika.

Ugonjwa wa kisukari hutokea pale kongosho (pancrease) inaposhindwa kutengeneza homoni au kichocheo aina ya Insulin, au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho.

Hali hiyo husababisha ongezeko la kiwango cha sukari kwenye damu (hyperglycemia).

Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Dkt Abdisalan anasema kuwa chakula kinapoyeyushwa matukio kadhaa hutokea ikiwa ni pamoja na sukari inayoitwa glucose ambayo ni chanzo cha nguvu mwilini kuingia katika damu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Tukio la pili hutokea katika kiungo kinachoitwa kongosho (pancrease) ambacho hutengeneza kichocheo cha Insulin.

Kazi ya Insulin ni kuondoa glucosei katika damu na kuingiza katika misuli, seli za mafuta na ini, ambako hutumiwa kama nishati.

Kuna aina mbili kuu ya ugunjwa wa kisukari,

Aina ya kwanza ya kisukari

Mtu hupatikana na aina hii ya kisukari ikiwa seli maalumu zinazotengeneza homoni ya insulin zinapokosekana katika tezi kongosho.

Pia kongosho zinapoharibika kutokana na sababu yeyote ile husababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Kwa mujibu wa wataalamu wa matibabu aina hii ya kisukari ni hatari sana.

Huwaathiri zaidi watoto na vijana

Aina ya pili ya kisukari

Katika aina hii ya kisukari, insulin huzalishwa kwa kiwango cha kutosha isipokuwa tatizo lipo kwenye ufanisi na utendaji kazi wake.

Haki miliki ya picha
Empics

Image caption

Upungufu wa mazoezi ni hatari kwa afya ya mwanadamu

Mara nyingi mtu hupatikana na aina hii kisukari ukubwani.

Hii inatokana na kupungua kwa utendaji kazi wa homoni ya insulin, au seli kushindwa kutumia insulin ipasavyo.

Hali hii mara nyingi husababishwa na unene uliopitiliza, au hali ya kutofanya mazoezi kabisa.

DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI

 • Kukojoa mara kwa mara
 • Kuhisi kiu kali na kunywa maji kwa kiwango cha kupitiliza (polydipsia).
 • Kuhisi njaa na kula mara kwa mara (polyphagia).
 • Kuchoka haraka
 • Kupungua uzito
 • Vipele mwilini
 • Kutoa harufu ya acetone inayofanana na harufu ya pombe.
 • kuhisi maumivu ya tumbo na kupoteza fahamu

Mtu anayeugua kisukari huwa na kiwango cha juu vya sukari kwenye damu kwa sababu mwili wake hauwezi kupeleka sukari kwenye seli za mafuta, ini na misuli ili ihifadhiwe kwa ajili ya kuzalisha nguvu.

Hali hali ya kuwa na kiwango cha juu cha sukari kwenye damu huenda ikaharibu moyo, macho, miguu na figo

Hata hivyo tiba maalum na uangalizi mzuri kwa watu wanaougua kisukari inaweza kuwahakikishia maishamarfu yenye afya.Source link

Zimbabwe bila ya Mugabe madarakani, hali ikoje?


Mnamo tarehe 14 Novemba jeshi likamuweka katika kifungo cha nyumbani kiongozi huyo mkongwe wa Zimbabwe, katika kujibu hatua ya Mugabe kumfukuza kazi makamu wake wa rais wakati huo Emmerson Mnangagwa. Mwaka mmoja tangu alipoondolewa madarakani Robert Mugabe, Je kuna mabadiliko yoyote?

Mamia kwa maelfu ya Wazimbabwe walicheza na kushangilia kwa furaha katika mitaa ya miji mbali mbali kusherehekea kumalizika kwa enzi ya utawala wa ukandamizaji wa Mugabe ambao ulichangia katika kuuharibu kabisa uchumi wa taifa hilo uliowahi wakati mmoja kuwa thabiti. Mugabe ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 92 alijiuzulu mara moja na kuumaliza utawala wake uliodumu miaka 37.

Mwaka mmoja baade matatizo ya kiuchumi ya Zimbabwe yameongezeka huku uhuru wa msingi ukiendelea kubanwa hali ambayo inawafanya baadhi ya wazimbabwe kujiuliza ni kitu gani hasa kilichobadilika? na je kuna ubora wowote? Ile furaha iliyokuweko Mugabe alipoangushwa madarakani imetoweka.Mnangagwa aliwaahidi Wazimbabwe ukurasa mpya lakini wengi nchini humo wanaonekana kubughudhika hasa bado inapoonekana misururu mirefu kwenye mabenki watu wakienda kutowa miburungutu ya pesa pamoja na upungufu mkubwa wa bidhaa za msingi ambao umechangia hata kuwepo hali ya mgao wa mafuta ya kupikia ,maji ya kunywa ya chupa pamoja na bia.

Simbabwe Protest in Harare (picture-alliance/AP Photo/B. Curtis)

Wananchi wa Zimbabwe wakiimba na kushangilia kumshinikiza Mugabe kuachia madaraka, 2017

Mkaazi mmoja wa Harare kwa jina Andrea Magoronye anasema walidanganywa,na kuandamana pasipo sababu ya msingi.Marogoye ni mkaazi wa mji mkuu Harare anazungumza hayo akiwa amesimama kwenye msururu mrefu wa kusubiri kununua mafuta ya kupikia kwenye duka la Supermarket.

Mnangagwa alianza vizuri uongozi wake lakini ushindi wake uliozusha utata katika uchaguzi mnamo mwezi Julai mwaka huu ulifuatiwa na hatua za jeshi kufyetua risasi na kuua watu sita,raia wasiokuwa na hatia.Mripuko wa Cholera ulifuatia na hali ngumu ya kiuchumi  ndo kwanza imezidisha mashaka juu ya uongozi wa mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 76 katika mwaka wake wa kwanza madarakani.

Mnangagwa aliaahidi kuugeuza uchumi ulioporomoka wa Zimbabwe kuwa wa kiwango cha kati kufikia mwaka 2030 ,kuanzisha msingi wa mageuzi ya demokrasia,na kujisogeza tena katika ushirikiano na Marekani pamoja na nchi nyingine za Magharibi ambazo ziliiweka Zimbabwe chini ya vikwazo wakati wa Mugabe. Vikwazo hivyo bado havijaondolewa na hakuna ishara zinazoonesha uhakika wa hilo kutokea. Mnamo mwezi Septemba mfumko wa bei za bidhaa ulipanda na kufikia kiwango cha juu zaidi ambacho hakijawahi kuonekana tangu mwaka 2010 kwa mujibu wa shirika la kitaifa la takwimu Zimstat.

Simbabwe Wahlkampf Präsident Mnangagwa (Reuters/P. Bulawayo)

Rais Emmerson Mnangagwa akiwasalimu wafuasi kwenye mkutano wa kampeni

Kuna upungufu wa dawa katika nchi nzima ambayo toka hapo mfumo wake wa afya umekwisha karibia kusambaratika muda mrefu. Maduka ya dawa ya binafsi yenye dawa yanauza dawa zao kwa dolla za kimarekani,fedha ambazo hazipatikani kirahisi nchini Zimbabwe.

Zimbabwe inaondokana taratibu na mripuko wa maradhi ya kipindupindu ugonjwa ambao rais ameutaja kama ni ugonjwa wa kizamani ambao umeshawauwa takriban watu 50 katika mji mkuu Harare. Wengi wanahofia  mgogoro wa sasa umechochewa na upungufu wa fedha za kigeni pamoja na kuongezeka kwa deni la nchi na kwa mujibu wa shirika la fedha duniani IMF hali hiyo huenda ikawa mbaya zaidi na kugeuka kuwa mgogoro wa kiuchumi ambao haujapata kuonekana kwa kipindi cha muongo mmoja nchini Zimbabwe, pale ambapo mfumko wa bei ulifikia asilimia billioni 500.

Juu ya hilo wanaomkosoa rais Mnangagwa wanasema serikali yake bado inawakandamiza watu huku ikitajwa kwamba kuna watu chungunzima waliokamatwa kwa tuhuma za kumkosoa rais,ukandamizaji ambao ni sawa na uliokuwa ukifanywa na utawala wa Mugabe.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri.Iddi Ssessanga

 Source link

Uingereza, EU wapata rasimu ya muafaka wa Brexit


Ofisi ya Waziri Mkuu May ilitangaza hapo jana kwamba wafanyakazi wa pande hizo mbili, Uingereza na Umoja wa Ulaya tayari wamekamilisha waraka wa muafaka huo.

Theresa May alikutana na mawaziri wake mmoja baada ya mwingine jana, na anatarajiwa kuitisha kikao cha baraza zima baadaye leo kuzungumzia muafaka uliofikiwa. Kulingana na msemaji wa serikali mjini London, amesema baraza la mawaziri ndilo litakaloamua hatua inayofuata.

Ikiwa baraza litaukataa muafaka huo uliofikiwa, Uingereza na Umoja wa Ulaya zitakuwa hazina makubaliano yoyote, huku tarehe ya mwisho ya Uingereza kuondoka rasmi katika Umoja wa Ulaya, tarehe 29 Machi 2019 ikikaribia.

Kizingiti katika baraza la mawaziri na bungeni

Kwa upande mwingine, ikiwa mawaziri watayaafiki makubaliano hayo, Uingereza itakuwa na nafasi nzuri ya kuitisha mkutano maalum wa Umoja wa Ulaya kuhusu Brexit, katika hatua za mwisho mwisho za kutalikiana na umoja huo.

UK Theresa May (Getty Images/C. McQuillan)

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha Jamhuri ya Ireland, makubaliano yamepatikana kuhusu mpaka baina ya Jamhuri hiyo na Ireland ya Kaskazini ambayo ni sehemu ya Uingereza. Mpaka huo umekuwa suala tete katika mazungumzo kuhusu Brexit.

Waziri Mkuu Theresa May amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka nani ya chama chake na katika baraza lake la mawaziri kuhusu suala hilo la mpaka wa Ireland.

Kizingiti kikubwa kinamsubiri Bi May katika bunge, ambako wajumbe wengi wametishia kuukataa muafaka huo ikiwa hautazingatia masuala yenye kipaumbele kwao.

Corbyn na Johnson 

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn amesema atasubiri kujua kikamilifu yaliyomo katika makubaliano yaliyofikiwa, lakini akaongeza kwamba ana mashaka ikiwa yatakuwa mema kwa nchi.

Mpinzani mkubwa wa Theresa May kuhusu mwelekeo wa Brexit, waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje, Boris Johnson ambaye anatoka chama cha Theresa May cha Conservative, ametishia pia kuyapinga makubaliano hayo, akimshauri Theresa May kuachana nao.

Katika kura ya maoni ya Juni 2016, asilimia 52 ya wapiga kura nchini Uingereza waliunga mkono Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: Daniel Gakuba/afpe, dpae

Mhariri: Caro Robi

 Source link

Uingereza, Umoja wa Ulaya wapata muafaka kuhusu Brexit


Ofisi ya Waziri Mkuu May ilitangaza hapo jana kwamba wafanyakazi wa pande hizo mbili, Uingereza na Umoja wa Ulaya tayari wamekamilisha waraka wa muafaka huo.

Theresa May alikutana na mawaziri wake mmoja baada ya mwingine jana, na anatarajiwa kuitisha kikao cha baraza zima baadaye leo kuzungumzia muafaka uliofikiwa. Kulingana na msemaji wa serikali mjini London, amesema baraza la mawaziri ndilo litakaloamua hatua inayofuata.

Ikiwa baraza litaukataa muafaka huo uliofikiwa, Uingereza na Umoja wa Ulaya zitakuwa hazina makubaliano yoyote, huku tarehe ya mwisho ya Uingereza kuondoka rasmi katika Umoja wa Ulaya, tarehe 29 Machi 2019 ikikaribia.

Kizingiti katika baraza la mawaziri na bungeni

Kwa upande mwingine, ikiwa mawaziri watayaafiki makubaliano hayo, Uingereza itakuwa na nafasi nzuri ya kuitisha mkutano maalum wa Umoja wa Ulaya kuhusu Brexit, katika hatua za mwisho mwisho za kutalikiana na umoja huo.

UK Theresa May (Getty Images/C. McQuillan)

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha Jamhuri ya Ireland, makubaliano yamepatikana kuhusu mpaka baina ya Jamhuri hiyo na Ireland ya Kaskazini ambayo ni sehemu ya Uingereza. Mpaka huo umekuwa suala tete katika mazungumzo kuhusu Brexit.

Waziri Mkuu Theresa May amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka nani ya chama chake na katika baraza lake la mawaziri kuhusu suala hilo la mpaka wa Ireland.

Kizingiti kikubwa kinamsubiri Bi May katika bunge, ambako wajumbe wengi wametishia kuukataa muafaka huo ikiwa hautazingatia masuala yenye kipaumbele kwao.

Corbyn na Johnson 

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Leba, Jeremy Corbyn amesema atasubiri kujua kikamilifu yaliyomo katika makubaliano yaliyofikiwa, lakini akaongeza kwamba ana mashaka ikiwa yatakuwa mema kwa nchi.

Mpinzani mkubwa wa Theresa May kuhusu mwelekeo wa Brexit, waziri wa zamani wa mambo ya nchi za nje, Boris Johnson ambaye anatoka chama cha Theresa May cha Conservative, ametishia pia kuyapinga makubaliano hayo, akimshauri Theresa May kuachana nao.

Katika kura ya maoni ya Juni 2016, asilimia 52 ya wapiga kura nchini Uingereza waliunga mkono Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya.

Mwandishi: Daniel Gakuba/afpe, dpae

Mhariri: Caro Robi

 Source link

Khashoggi: Uturuki yaendelea kuishutumu vikali SaudiaJumanne, gazeti linalomilikiwa na serikali ya Uturuki liitwalo Sabah, lilichapisha picha za X-Ray na kudai kwamba zilionyesha vifaa vilivyotumika kwa mauaji ya Khashoggi, vikiwa ndani ya sanduku lililobebwa na watu waliokuwa wametoka Saudi Arabia.

Ripoti iliyoandikwa kwenye gazeti hilo, imetajwa na wachambuzi kama hatua ya hivi karibuni kabisa ya kampeni kabambe iliyopangwa na Ankara dhidi ya Riyadh, ikikusudiwa kuwafichua waliohusika kwa kifo cha mwandishi huyo, aliyekuwa mosoaji mkubwa wa utawala wa ufalme wa Saudia.

Wiki jana, Rais Erdogan alisema kwamba sauti zilizorekodiawa wakati Khashoggi aliuawa, zimetumwa kwa Marekani, Saudi Arabia, na nchi zingize zenye nguvu za bara ulaya.

Tangu kuuawa kwa Khashoggi tarehe mbili mwezi uliopita, Ankara, kwa taratibu, imekuwa ikitoa ripoti kwa vyombo vya habari juu ya yale inayosema yalitukia kwenye ubalozi huo mdogo.

Wachambuzi wanasema utaratibu huo wa kutoa habari kila baada ya muda fulani, umedumaza matuamaini ya Riyadh kwamba gumzo kuhusu sakata hiyo, litafifia.

Mwana wa mfalme wa Saudia, Mohamed Bin Salman, ambaye anashutumiwa kuhusika kwa sakata hiyo, ameendelea kukanusha kwamba ufalme ulihusika kwa vyovyote katika mauaji hayo.Source link

Meenakshi Valand: "Nilitaka kuwa na mtoto wangu mwenyewe na sikutaka kutumia mbinu nyingine yoyote."


Haki miliki ya picha
Galaxy Care Hospital

Image caption

Meenakshi Valand ni mwananamke wa 12 duniani kujifungua mtoto baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi

Meenakshi Valand ni mmoja kati ya watu wachache duniani ambao wamejaaliwa kupata watoto ibaada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.

Alikuwa na furaha isiyokuwa na kifani.

“Sikuweza kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni machozi ya furaha – Nimepoteza watoto sita katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita,” aliiambia BBC.

Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliyopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mamake mzazi.

Katika miaka tisa ya ndoa yake, Meenakshi alipoteza watoto wawili kutokana na tatizo katika mfuko wake wa uzazi.

Hali hiyo inajulikana kama Ashermans syndrome.

Lakini hakukata tamaa. “Nilitaka kuwa na mtoto wangu mwenyewe. Sikutaka kutumia mbinu nyingine yoyote.”

Kwa mujibu wa jarida la kimataifa la utatafiti wa kisayansi, 15% ya watu hawana uwezo wa kuzaa na 3 kati ya 5% ya visa hivi husbabishwa na matatizi ya mfuko wa uzazi.

Haki miliki ya picha
Galaxy Care Hospital

Image caption

Radha alizaliwa Oktoba kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45

Alimtembelea Dkt Shailesh Putambekar, mtaalamu wa upasuaji na upandikizaji wa mfuko wa uzazi katika hospitali ya Galaxy Care mjini Pune.

Wakati huo mama yake Sushila Ben alikuwa amejitolea kupatia mfuko wake wa uzazi ili kumuezesha kupata mtoto.

Upandikizaji huo ulifanywa na kundi la wataalam 12 mwezi Mei mwaka 2017 na ulifanikiwa.

Lakini Januari mwaka huu alikabiliwa na changamoto nyingine baada ya hatua ya kuhamisha kijisu kukwama.

Hata hivyo utaratibu huo ulifanywa tena mwezi Aprili.

Wiki 20 baadae mwanawe Radha alizaliwa kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45.

Dkt Putambekar alisema , “Meenakshi alianza kupata kupata matatizo mengine ikiwa ni pamoja na shinikizo la damu hali ambayo aliwalazimu kumfanyia upasuaji wa dharura ili kumuokoa mama na mtoto.

Mtoto alizaliwa salama lakini kabla ya wakati na alikuwa na kilo 1.45 ”Lakini anaendelea vizuri hana neno”

Hii ilikuwa mfumu wa kwanza wa kuzalisha ambao ni wa 12 kote duniani.

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi enzi hizi:

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kisa cha kwanza mtoto kuzaliwa kupitia upandikizaji wa kizazi kilifanyika nchini Uswidi mwaka 2014

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi umefanywa katika mataifa 10 ikiewemo: Uswidi, Saudi Arabia, Uturuki, Marakani, Uchina na Jamhuri ya Czech, Brazil, Ujerumani, Serbia na India.

 • 2014 – Mwanamke kutoka mji wa Gothenburg, nchini Uswidi alijifungua mtoto wa kiume kupitia utaratibu wa kupandikizwa mfuko wa uzazi.
 • Mwanamke huyo wa miaka 36 alipata mhisani wa miaka 60 aliyempatia kizazi.
 • 2017 – Mwanamke katika mji wa Dallas, Texas, alizaa mtoto kupitia mfumo wa upandikizaji wa mfuko uzazi nchini Marekani.
 • 2018 – Mwanamke alifanikiwa kujifungua mtoto wa msichana kupitia upandikizaji wa mfuko wa uzazi kwa mara ya kwanza nchini India.
 • Watoto 12 wamezaliwa kupitia mfumo huo nane kati ya watoto hao wamezaliwa nchini Uswidi.
 • Ni mwanamke mmoja tu kati ya 12 aliyepandikizwa kizazi cha mtu aliyekufa

Mfumo huu unafanya kazi vipi?

Wakati wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi mfumo wa neva haupandikizwi kwa hivyo mwanamke hapati uchungu wakati wa kujifungua mtoto.

Mfumo huu maalum ulipoanza ulikuwa ukichukua hadi saa 13 kufanywa. “Lakini sasa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unachukua saa sita anasema Dkt Shailesh Puntambekar.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mfumo wa upandikizaji wa kizazi umefanyika katika mataifa 10 kufikia sasa

Kwa mujibu wa kundi la wataalamu katika hospitali ya Galaxy Care, mfumo wa upandikizaji wa mfuko wa uzazi unagharimu karibu dola 11000.

Lakini katika kesi ya Meenakshi Wayanad ambayo ni ya kwanza na aina yake nchini India, hakutakiwa kulipa chochote.

Alipewa dawa za kudhibiti mfumo wa kinga mwilini ili kuzuia mfuko mpya wa uzazi kukataliwa.

Mwaka mmoja baada ya upandikizaji, madkatari waliamua kupandikiza kijusi kilichokuwa kimegandishwa.

Wanasema upandikizaji unadhaniwa kuwa salama kwa mama na mtoto licha ya kutumiwa kwa dawa inayofahamika kama (immuno-suppressants) pomoja na kuhusishwa kwa upasuaji wa aina tofauti.

Nchini India pekee karibu wanawake 600 wamewekwa katika orodha ya watu wanaotaka kufanyika upandikizaji wa kizazi kipya

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Awali njia ya pekee ambayo mwanamke aliye na tatizo la kizazi kupata mtoto ni kupitia mfumo wa kibiologia ambapo mwanamke mwingine anatumiwa kubeba mimba kwa niaba ya yule aliye na tatizo la kushika mimba

Uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi umebaini kuwa utaratibu huo umepata ufanisi mkubwa lakini unahitaji majaribio ya kliniki ya kudhibiti kisaikolojia na ukaguzi katika ngazi kadhaa.

Wakichangia katika jarida la kimataifa la masuala ya uzazi kundi la madaktari kutoka Japan limesema huku utaratibu wa kupandikiza mfuko wa uzazi ukisifiwa kwa kuwapa faraja wanawake waliyo na tatizo la mfuko wa uzazi bado utaratibu huo unaendelea kufanyiwa majaribio.

Matumaini ndiyo kitu Meenakshi alikuwa akijipatia: “Nimeteseka sana lakini sasa nina furaha kupita maelezo.”Source link

Mzozo wa Palestina na Israel: watatiza Baraza la Usalama


Shambulio lililofanywa na Israel Ukanda wa Gaza

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Shambulio lililofanywa na Israel Ukanda wa Gaza

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kukubaliana na mwenendo wa ghasia zilizotokea hivi karibuni kati ya Israel na Palestina katika Ukanda wa Gaza.

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour ameilaumu Marekani kwa kuwa kipingamizi.

Mapigano makali kuwahi kutokea katika kipindi cha muda wa miaka minne, yaliibuka siku ya Jumapili iliyopita baada wa wapiganaji wa Hamas kuingilia kati operesheni za siri zilizokuwa zikifanywa na Israel katika ukanda wa Gaza.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mama wa mmoja wa Makamanda wa Hamas akilia kwa uchungu, baada ya mwanawe kuuawa

Chama cha Wapalestina cha Hamas kimesema kinachunguza kama Isreael imezingatia makubaliano ya Misri ya kusitisha mapigano.

Kwa upande wake Israel nayo imesema itaendelea na mashambulio yake ya anga katika ukanda wa Gaza ikiwa ni lazima kufanya hivyo.

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Danny Danon amesema nchi yake kila siku inafanya kila liwezalo kuhakikisha usalama wa watu wake.

”..Tunachukua hatua kuwalinda watu wetu. Na wakati unapojua kwamba kuna mtu anachimba njia ya chini ya ardhi ama kuna mtu anapanga mashambulizi ama tukio la utekaji, utachukua hatua za kujilinda.

Tutaendelea kuchujua hatua hizo, haijalishi zitafanyika wapi kwa ajili ya kuwalinda watu wetu na mashambulizi yajayo…” Amesema Danon

Katika mapigano hayo Wapalestina sita waliuawa na mashambulizi yaliyofanywa na Israel, huku roketi zilizorushwa na wapiganaji wa Hamas zikiua muisrael mmoja.Source link