DCJ: Philomena Mwilu: Kesi ya Naibu Jaji Mkuu yasimamishwa Kenya


Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)

Haki miliki ya picha
YASUYOSHI CHIBA

Image caption

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu (Katikati)

Mahakama Kuu Kenya imesimamisha uendeshaji wa kesi ya ufisadi dhidi ya Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu.

Mwilu amewasilisha ombi katika mahakam hiyo akiomba asijibu mashtaka ya ulaghai, utumiaji mbaya wa mamlaka na kukwepa kulipa kodi, kesi iliyowasilishwa dhidi yake hapo jana na mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma.

Alikamatwa Jumanne katika majengo ya Mahakama ya Juu zaidi na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu ambapo baadaye aliachiliwa huru kwa dhamana.

Kupitia wakili wake, Okongo Omogeni, Mwilu ameambia Mahakama Kuu leo asubuhi kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa dhidi yake ina hila na ni njama dhidi yake.

Katika ombi lake mahakamani, alikuwa amewashtaki mkurugenzi wa mashtaka ya umma, Idara ya Uchunguzi wa Jinai, Mwanasheria Mkuu na Hakimu Mkuu anayeangazia kesi za ufisadi.

Image caption

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji

Mahakama ya juu sasa imeamua kusitisha kesi ya uhalifu inayomkabili Mwili kukisubiriwa kuamuliwa masuala ya kikatiba yanayotokana na ombi alilowasilisha Okotoba 9.

Jaji Chacha Mwita wa mahakama kuu ameeleza kwamba ombi hilo la Mwilu linazusha masuali makuu.

Naibu jaji mkuu huyo anakabiliwa na mashtaka kadhaa yakiwemo kutumia vibaya mamlaka yake, na kutolipa ushuru.

Inadaiwa kuwa jaji huyo alikiuka sheria ya uongozi na maadili kwa kupokea mkopo wa kibinafsi wa thamani ya takriban $120,000 kutoka kwa benki ya Imperial.

Mwilu hatahivyo amejitetea kwa kusema mkopo huo ulitokana na makubaliano ya kibiashara.

Mahakama hiyo kuu imeamua sasa kwamba kuna masuala ya kutathminiwa kikatiba kubaini iwapo makubaliano ya kibiashara baina ya mtu na taaisis ya kibiashara yanaweza kutazamwa kama mashtaka ya uhalifu.

Kwa sasa kesi hiyo ya uhalifu imesimamishwa hadi Oktoba 9.

Hatua hii ina maana gani kisheria?

“Mawakili wa jaji Mwili waliuliza je kuna kosa la jinai katika kukosa kulipa ushuru? ushuru si kazi ya polisi bali kazi ya Kenya Revenue Authority, yaani kile kitengo cha Kenya cha kukusanya ushuru. Kwa hivyo hilo ndilo tetesi la kwanza. Tetesi la pili ambalo walichukua pale mahakamani ni kwamba naibu jaji mkuu alichukua mkopo kutoka benki na hakuweza kupeana dhamana, wakauliza makubaliano ya benki na kupeana taratibu za kutoa mkopo ni vitu ambavyo havimo mikononi mwa polisi. Kwa hivyo hayo maswali mawili ndiyo yaliulizwa pale kotini na kusema kuwa yale mashtaka yanakiuka kanuni za kikatiba,” kulingana na mwanasheria Danstan Omari alipozungumza na BBC.

Hata hivyo kesi ilisimamishwa kufuatia kuwepo dosara kwenye namba za faili za kesi. Kesi hiyo sasa imesimamishwa hadi tarehe tisa mwezi Oktoba. Hii ina maana kuwa jaji Mwilu yuko huru kuendelea na kazi zake kama kawaida akisubiri uamuzi wa mahakama ya juu. Baada ya dhamana yake aliyoweka mahakamani kukamilika siku ya Ijumaa atakuwa tena huru kuendelea na kazi zake kama naibu jaji mkuu.Source link

Sakata la Korosho: Je, shinikizo la kisiasa limemng'oa Hawa Ghasia Kamati ya Bajeti?


Ghasia akitoka kuhutubia mkutano na wanahabari

Haki miliki ya picha
CCM

Image caption

Hawa Ghasia na Jitu Soni wamejiuzulu uongozi wa kamati ya bunge ya bajeti bila kutoa maelezo juu ya uamuzi wao.

Maswali na mjadala umeibuka juu ya hatua ya kujiuzulu viongozi wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, mwenyekiti Hawa Ghasia na naibu wake Jitu Soni.

Ghasia ambaye ni mbunge wa Mtwara Vijijini na Soni mbunge wa Babati Vijini wote kupitia chama tawala CCM walitangaza uamuzi wao mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jana Jumanne asubuhi jijini Dodoma bila kutoa sababu za kufikia maamuzi hayo tena kwa pamoja.

BBC ilifanya jitihada za kuzungumza na Bi Ghasia na kutaka atumiwe ujumbe mfupi ambao hata hivyo hakuujibu.

Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai ameliambia gazeti la kila siku la Kingereza Tanzania The Citizen kuwa ofisi yake licha ya kupokea taarifa za kujiuzulu nyadhifa za wabunge hao lakini hawana taarifa juu ya sababu ya uamuzi huo.

Bi Ghasia hatahivyo hwa ufupi kabisa aliliambia Gazeti la Mwananchi kuwa,”Mimi nimejiuzulu kwa hiari yangu, sitaki kuzungumza na waandishi wa habari, ‘full Stop’. Mbona nilivyochaguliwa hamkuja kunihoji nini malengo yangu lakini sasa nimemaliza mnataka kunihoji.”

Kamati ya Bajeti ambayo inanguvu ya kikanuni kuibana serikali katika masuala ya kibajeti chini ya uongozi wa Bi Ghasia itakumbukwa kwa namna ilivyoibana serikali katika vipindi tofauti ikitaka mabadiliko ya kibajeti.

Haki miliki ya picha
ushirika

Image caption

Zao la korosho linazalishwa kwa wingi kusini mwa Tanzania

Mwezi Juni mwaka huu kamati hiyo iliongoza wabunge bila kujali tofauti zao za kisiasa katika kupinga mapendekezo ya serikali katika Sheria ya Fedha wa mwaka 2018 kwa kuchukua asilimia 100 ya tozo za mauzo ya korosho nje ya nchi (Export levy) kupelekwa mfuko mkuu wa fedha za serikali.

Awali, asilimia 65 ya tozo hiyo ilikuwa ianenda kwenye mfuko wa zao hilo na baadae kurejeshwa kwa wakulima kupitia pembejeo. Hoja ya wabunge wakiongozwa na kamati ya bajeti ilikuwa, hatua ya kuchukua fedha zote ingeleta athari kubwa kwa maendeleo ya zao hilo na wakulima wake.

Mjadala ukawa mkali lakini hoja ya serikali ikapita. Baadae, Rai John Magufuli akasema hakupendezwa na namna ya wabunge wa CCM hususani wa mikoa ya kusini kwa namna walivyolijadili suala hilo, na akatishia kuwa laiti wangeliandamana basi angetuma askari wawaadhibu.

Kutokana na mjadala wa korosho, wadadisi wa masuala ya kisiasa na baadhi ya wabunge wakausifu msimao wa Ghasia na kamati yake.

Akizungumzia juu ya kujiuzulu kwa Ghasia Mbunge wa Kigoma Mjini ACT Zitto kabwe kupitia ukurasa wake wa twitter alisema, “Nimesikitishwa sana na uamuzi Huu. Kamati ya Bajeti ya Hawa Ghasia ilikuwa imeanza kurejesha heshima ya Bunge. Ndio Siasa za zama hizi. Asante sana Hawa kwa kazi uliyofanya.”

Je, kuna shinikizo la kisiasa?

Kuna ambao wanaamini kuwa viongozi hao wameshurutishwa kujiuzulu kutokana na msimamo wao imara juu ya sakata la korosho.

Gazeti la Mwananchi limedai kudokezwa na chanzo ambacho hawakukutaja jina kuwa uamozi wa Ghasia na Soni haukuwa wa hiyari. Huku mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kupitia mtandao wake wa twitter pia ameashiria kuwa kulikuwa na shinikizo.

“Mkti Kamati ya Bajeti ya Bunge Hawa Ghasia /Makamu wake wamejiuzulu Uongozi kwa ridhaa yao ?ebu tuone huko mbele ya safari,pengine vichwa vya habari vitakuja kubadilika na kusema Hawa Ghasia na Makamu wake watakiwa kujiuzulu Uongozi Kamati ya Bajeti ya Bunge.Najaribu kuwaza tu,” aliandika Lema.

Mwezi Machi 2017, mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Dk Dalali Kafumu na makamu wake, Vicky Kamata kwa pamoja walitangaza kujiuzulu nafasi zao.

Wawili hao hata hivyo hawakuficha sababu zao kwa kuweka wazi kuwa walichukua uamuzi huo kutokana na Serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi.

Baada ya kujiuzulu kwa Ghasia na Soni, , wajumbe wa kamati ya bajeti walimchagua mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene kuwa mwenyekiti na mbunge wa Maswa Magharibi, Mashimba Ndaki kuwa makamu, wote wawili ni kutoka upande wa CCM.Source link

Mauaji ya kimbari: Ujerumani yarejesha mafuvu ya watu iliowaua Namibia 1904


Herero woman in traditional dress

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mwanaharakati wa Herero Esther Muinjangue bado anataka msamaha kutoka serikali ya Ujerumani

Ujerumani imerejesha mabaki ya binadamu ya watu wa asilia waliouawa wakati wa mauaji ya kimbari wakati wa ukoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.

Ujumbe wa serikali ya Namibia ulipokea mafuvu hayo wakati wa ibada ya kanisa kwenye mji mkuu Berlin.

Mifupa hiyo ilikuwa imetimwa kwenda Ujerumani kufanyiwa utafiti kubaini uwezo wa wazungu.

Maelfu ya watu wa Horero na Nama waliuawa walipokuwa wakipinga ukoloni.

Vizazi vyao bado vinasubiri msamaha kutoka kwa serikali ya Ujerumani.

Kwa nini mauaji hayo yakatokea?

Mauaji hayo yalianza mwaka 1904 baada ya jamii za Herero na Nama kuasi baada ya wajerumani kuchukua mashamba yao na mifugo.

Mkuu wa jeshi wa ile iliyojulikana kama German South West Africa, Lothar von Trotha alitoa amri ya kuuliwa watu Oktoba mwaka 1904.

Herero na Nama walisukumwa kwenda jangwani na yeyote ambaye alipatikana akirudi kwenda kwa ardhi yao aliuawa au kupelekwa kwenye zenye misongamano.

Haki miliki ya picha
Hulton Archive

Image caption

Wanajeshi wa Ujerumani waliuaa wakabaka na kuwafanya watu watumwa

Hakuna idadi kamili ya watu waliouawa na makadirio mengine yamewekwa kuwa takriban watu 100,000.

Inaaminiwa kuwa asilimia 75 ya watu wa Horero na nusu ya watu wa Nama walikufa.

Mafuvu ya baadhi ya wale walio uawa yalitumwa kwenda nchini Ujerumani ambapo wasayansi waliyafanyia uchunguzi kama njia ya kubaini ukweli kuhusu uwezo wa wazungu.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mafuvu yalikuwa sehemu ya mabaki ya binadamu yaliyofanyiwa utafiti nchini Ujerumani

Inaamiwa kuwa kuna mamia ya mafuvu ya raia wa Namibia nchini Ujerumani na leo Jumatano zaidi ya mafuvu 25 yalisalimishwa.

Mafuvu kutoka koloni zingine za Ujerumani zikiwemo Cameroon, Tanzania, Rwanda na Togo yalitumwa kwa utafiti huo.

Ujerumani itaomba msamaha?

Mwaka 2016 Ujerumani ilisema ilikuwa inajiandaaa kuomba msamaha lakini bado inajalidiliana na serikali ya Namibia njia ya kuomba msamaha huo.

Sherehe ya leo Jumatano ndiyo mara ya tatu ambapo mabaki yanarejeshwa Namibia lakini kulikuwa na matumaini kuwa mara hii kungekuwa na mapatano kamili.

Vizazi vya waathiriwa vina machungua kuwa hukujakuwepo msamaha na makubaliano ya fidia. Pia wana hasira kuwa hawajashirikishwa kweney mapatano hayo.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mabaki hayo sasa yatapelekwa nchini NamibiaSource link

Ghasia za kibaguzi zaibuka tena Afrika Kusini


Vitendo vya ubaguzi wa rangi vimeibuka tena Afrika kusini

Image caption

Vitendo vya ubaguzi wa rangi vimeibuka tena Afrika kusini

Polisi nchini Afrika kusini wamethibitisha vifo vya watu wawili katika mapigano yaliyotokea kati ya wenyeji na wageni katika mji wa Soweto.

Katika ghasia hizo maduka yanayomilikiwa na wageni yaliporwa bidhaa, wakati vurugu zilipotapakaa eneo lote.

Ghasia za kupinga wahamiaji zimekuwa zikijitokeza nchini Afrika kusini, hali inayosababishwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira na umasikini.

Vurugu zinazochochea uporaji wa vitu zimesambaa katika maeneo mengi ya Soweto.

Kwanini kiongozi wa Kamati ya Bunge Tanzania amejiuzulu?

Ujerumani yarejesha mafuvu ya watu iliowaua Namibia 1904

zilianzia katika duka moja, baada ya wakazi wa eneo hilo kumtuhumu mmiliki wa duka mwenye asili ya Somalia kumshambulia kwa risasi na kumuua kijana mdogo aliyedai kuwa alikuwa akijaribu kuvunja duka lake.

Polisi nchini humo wana amini kwamba tukio hilo ndio lililozua mtafaruku na kusababisha ghasia ambazo sasa zimesambaa katika maeneo kadhaa ya mji huo.

Wakazi hao pia wanawalaumu wamiliki wa maduka, ambao wengi ni wageni, kuuza vyakula vilivyopitwa na wakati.

Image caption

Maduka yanayomilikiwa na wageni Afrika kusini

Ujumbe wa WhatsApp umekuwa ukizunguuka nchini Afrika kusini ukimuonya yeyote yule, aliyepangisha vyumba kwa Wasomali, awafukuza.

Kwa mujibu wa ujumbe huo iwapo hawatafanya hivyo mpaka ifikapo tarehe 8 Septemba nyumba zote na maduka yatachomwa moto.

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.08.2018

Idadi ya maduka haya yanayomilikiwa na wageni yamejengwa katika maeneo ya karibu na makazi na yamekuwa yakimilikiwa raia pia kutoka nchi nyingine kama vile Ethiopia, Zimbabwe na Pakistan.

Hali hiyo pia imewafanya wamiliki wengi wa maduka kufungasha bidhaa zao na kuondoka mjini humo wakihofia vurugu zaidi.Source link

Bobi Wine: Awakilishwa na wakili wake mahakamani Uganda


Bobi Wine akiwa mahakamani kabla ya kuachiwa kwa dhamana.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana Jumatatu wiki hii baada ya kuwekwa kizuizini na jeshi la Uganda ambapo inaripotiwa aliteswa.

Mbunge wa Uganda na msanii Bobi Wine hakuhudhuria kikao cha mahakama hii leo kuhusiana na kesi ya uhaini iliowasilishwa dhidi yake na serikali.

Mmoja wa mawakili wake Tonny Kitara anasema kuwa Bobi Wine bado amelazwa katika hospitali moja mjini Kampala kufuatia majeraha aliyopata wakati alipokamatwa na wanajeshi.

Mwanamuziki huyo anatarajiwa kusafirishwa kwa matibabu ijapokuwa haijulikani anatarajiwa kupelekwa wapi.

Watu 25 waliokuwa wameshtakiwa pamoja naye katika mahakama ya hakimu mkuu mjini Gulu waliwasili mahakamani humo kaskazni mwa Uganda kulingana na bwana Kitara.

Jumla ya watu 33 wameshtakiwa na uhaini kufuatia madai kwamba waliupiga mawe msafara wa rais Yoweri Museveni.

Baadhi ya washukiwa hao hawakuonekana mahakamani kwa sababu ya hali mbaya ya kiafya ama mkanganyiko wa siku ya kusikizwa kwa kesi hiyo .

Stakhabadhi zao za dhamana kwa makosa zilisema kuwa wanatarajiwa kuwasili mahakamani Septemba 30 na sio Agosti 30. Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe mosi Oktoba.

Baadhi ya washitakiwa wanaendelea kupata matibabu hospitalini na huenda wakashindwa kuhudhuria mahakamani ambapo watawakilishwa na mawakili wao.

Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi ni mwakilishi wa eneo bunge la Kyadondo Mashariki na ni msanii maarufu wa muziki nchini Uganda.

Alikamatwa wiki mbili zilizopita kwa tuhuma za uvamizi wa msafara wa Rais Museveni mjini Arua na kupokea kipigo kikali yeye na wenzie 32 kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Dereva wa Bobi Wine alipigwa risasi na kuuawa katika purukushani hizo.

Watuhumiwa hao waliwekwa chini ya ulinzi wa jeshi huku Bobi Wine awali akipandishwa katika mahakama ya kijeshi kwa tuhuma za kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Rais Yoweri Museveni alijitokeza na kukanusha taarifa kuwa Bobi Wine ameumizwa vibaya na kuvishutumu vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo.

Baada ya kelele za upinzani kupazwa ndani na nje ya Uganda pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, kesi yake mbele ya mahakama ya kijeshi ilifutwa na kuachiwa huru kabla ya kukamatwa tena na kufunguliwa mashtaka ya uhaini katika mahakama ya kiraia.

Jumatatu wiki hii, Bobi Wine na washukiwa wengine wote waliachiwa kwa dhamana.Source link

Theresa May na mtihani wa Uingereza kuboresha biashara na Afrika baada ya kujitenga na Umoja wa Ulaya


Waziri mkuu Theresa May na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika ikulu Nairobi

Haki miliki ya picha
PA

Image caption

Waziri mkuu Theresa May na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika ikulu Nairobi

Uingereza ina uhusiano wa kihistoria na mataifa mengi ya Afrika. Uhusiano huo bado unaendelea kuwa na maana, lakini kitu kimoja ambacho Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekutana nacho katika ziara yake ya Afrika ni kuwa nchi yake inagombea nafasi na mataifa mengine yanayowekeza kwa kiwango kikubwa.

Hii leo Bi May ametua Kenya baada ya kuzuru Afrika Kusini na Nigeria. Hii ni ziara ya mwanzo kwa Bi May barani Afrika akiwa mamlakani. Nchi yake imenuwia kuimarisha mahusiano yake na mataifa ya Afrika kipindi hiki ambacho wanakaribia kujitenga na Umoja wa Ulaya (EU).

Akiwa jijini Cape Town, Bi May ameahidi nchi yake kuwekeza pauni bilioni 4 barani Afrika mara baada ya nchi yake kuondoka EU mwakani.

May pia amesema anatarajia kusain makubaliano na serikali ya Kenya kurejesha mabilioni ya pesa yaliyotoroshewa Uingereza kinyume cha sheria.

Haki miliki ya picha
PA

“Azma ya Uingereza baada ya kujitoa EU mwezi Machi 2019 ni kuimarisha ushirikiano wake na dunia kwa ujumla…Wiki hii natarajia kuwa na mjadala wa namna gani wa kufikia azma hiyo pamoja na bara la Afrika kwa kusaidia katika uwekezaji wenye tija na kukuza ajira pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama,” ilisema sehemu ya taarifa ya Bi May kabla ya ziara yake.

Hatahivyo, hilo linaweza kuwa jambo gumu.

Kabla ya May kuwasili Kenya, rais wa taifa hilo Uhuru Kenyatta alikuwa Marekani ambapo alifanya mazungumzo na rais Donald Trump na wawili hao kusaini makubaliano kadha ya kibiashara yenye thamani ya $900 miloni.

Baada ya kukutana na Bi May, Bw Kenyatta ataelekea Uchina kwenda kushiriki mkutano wa uhusiano baina ya Uchina na Afrika.

Haki miliki ya picha
MICHAEL KHATELI

Image caption

Mikopo ya Uchina ilifadhili mradi wa reli kutoka mji mkuu Nairobi haid Mombasa. Je Uingereza itatoa nini?

Uingereza kwa sasa inabadili sharia zake ili kuruhusu bidhaa kutoka Afrika zinaingia nchini humo kwa namna sawa kama ilivyo sasa hata baada ya kujitenga na EU.

Uingereza yajaribu kuivutia Afrika baada ya Brexit

Nchi za Afrika, nyingi zikiwa makoloni ya zamani ya Uingereza zitalazimika kujipanga upya katika uhusiano wao na nchi hiyo hususan baada ya kujitenga na EU. Endapo Uingereza itashindwa kuafikiana vizuri na EU kabla ya pande hizo mbili kutengana basi ni Dhahiri uhusiano wa kibiashara baina ya Uingereza na Afrika pia utayumba.

“Kenya mathalan mzunguko wake wa biashara baina ya EU na Uingereza ni asilimia 50 kwa 50, hivyo basi inawabidi waingie makubaliano mazuri na pande zote mbili sababu inahitaji masoko yote hayo kuuza chai, bidhaa ghafi na mazao mengine,” mchumi Tony Waitima ameiambia BBC.

Kenya ndio nchi kinara kwa kuuza maua waridi (roses) katika Umoja wa Ulaya, na ni nchi ya tatu kwa kuuza maua kwa ujumla duniani. Kilimo cha maua kinategemewa moja kwa moja na watu 500,000 kwamujibu WA Baraza la Maua la Kenya hivyo kupata makubaliano mazuri kutoka pande zote mbili ni jambo muhimu zaidi.

Pamoja na juhudi za Uingereza kuishika Afrika kibiashara lakini ni wazi kuwa bara hilo kwa sasa linabembelezwa kutoka kila kona.Source link

Trump: Mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini yatakuwa makubwa zaidi


Donald Trump

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Ni sabubu ya China asema Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameikosoa China kwa kuhujumu jitihada zake na Korea Kaskazini, wakati kuna malalamiko kuhusu maendeleo ya kuharibu silaha za nyuklia za Korea Kaskazini.

Kupitia ujumbe wa Twitter alisema hakuna sababu ya kutoendelea tena na mazoezi ya kijeshi na Korea Kusini ambayo yamekuwa yakiikasirisha Korea Kaskazini.

Siku zilizopita waziri wake wa ulinzi alisema mazoezi ya kijeshi yanaweza kuendelea.

China imeikosoa Marekani kwa kuilaumu kuhusu uhusiano wake na Korea Kaskazini.

Mkutano kati ya Bw Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-un mwezi Juni ulikamilika kwa ahadi kutoka Korea Kaskazini kufanya kazi katika kuharibu silaha za nyuklia kwenye rasi na Korea.

Baadaye Trump alitangaza kuwa hakukuwa tena na tisho kutoka Korea Kaskazini.

Lakini tangu wakati huo waangalizi wengi wanasema kuwa Korea Kaskazini haifanyi hima katika kuharibu maeneo yake ya kurushia makombora.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Trump alisema tatizo limetatuliwa baada ua mkutano na Kim Jong-un ,mwezi Juni.

Kwa nini anailaumu China?

Kwenye matamshi yake kupitia Twitter, Bw Trump anasema Korea Kaskazini iko chini ya shinikizo kutoka China kwa sababu ya mvutano wa kibiashara kati ya Marekani na serikali ya China.

China ndiyo mshirika pekee wa Korea Kaskazini na inatajwa kuwa na ushawishi mkubwa kwenye maamuzi yake. China pia ndiye mshindani mkubwa wa Marekani na wa muda mrefu eneo hilo.

Marekani na China ziko kwenye mvutano mkuwa wa kibiashara na kila upande umeziwekea ushuru bidhaa za mwingine.

Hatua gani zimepigwa katika kuharibu silaha za nyuklia?

Tangu mkutano wa Juni, Korea Kaskazini imesitisha majaribio yake ya nyuklia, ikidai kuharibu kituo cha kufanyika majaribio ya nyuklia na ikarudisha mabaki ya wanajeshi wa Marekani waliouawa wakati wa vita vya Korea kati ya mwaka 1950-53.

Bw Trump ameilaumu Korea Kaskazini kwa kile amekitaja kuwa kutokuwepo hatua katika makubaliano yake ya kuharibu silaha za nyuklia.

Ripoti ya hivi majuzi ya Vox ilisema Korea Kaskazini ilijikokota kusonga mbele baada ya Trump kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa Bw Kim, kuwa angeweka sahihi mukubaliano ya kumaliza vita vya Korea.

Baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kupata kuwa Korea Kaskazini ilikuwa inandelea na mipango yake ya nyuklia, Marekani iliitaka jamii ya kimaifa kudumisha vikwazo vya kiuchumi na Korea Kaskazini.

Haki miliki ya picha
KCNA

Image caption

Korea Kaskazini ilifanya majaribio kadhaa ya makombora mwaka 2017

Mazoezi ya kijeshi yatarudi?

Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea yameikasirisha kwa siku nyingi Korea Kaskazini.

Kufuatia mkutano wa Juni Bw Trump alisimamisha mazoezi hayo ya kijeshi.

Katika ujumbe wake wa hivi majuzi, rais wa Marekani alisisitiza kuwa uhusiano wake na Kim ulibaki kuwa mzuri na hakukuwa na sababu ya kuanzisha tena mazoezi ya kijeshi na Korea Kaskazini.

Lakini aliongeza kuwa ikiwa yataanza yatakuwa makubwa kuliko yoyote yale.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Wanajeshi wa Marekani na Korea Kusini wakifanya mazoezi

Tangu kumalizika vita vya Korea, wakati Marekani ilishirikiana na Korea Kusini kuipiga vita Korea Kaskazini, Marekani imekuwa na wanajeshi wake nchini Korea Kusini.

Karibu wanajeshi 29,000 wa Marekani wako nchini Korea Kusini chini ya makubaliano ya ulinzi yaliyofikiwa mwaka 1953.Source link

Wavuvi wanaotumia mipira ya kondomu kuimarisha usalama wao Mombasa Kenya


Simu

Image caption

Simu zilizotiwa ndani ya mipira ya kondomu

Miezi mitatu iliopita wavuvi sita katika pwani ya Kenya huko mjini Mombasa walipatwa na janga kubwa baada ya boti yao kuzama nyakati za usiku.

Wanne kati yao waliaga dunia baada ya wimbi kubwa kuwapiga muda mfupi baada ya ajali hiyo ya boti swala lililowafanya kutengana.

Kulingana na Matano Jafar ambaye ni mmoja wa manusura wa janga hilo yeye na mwenzake walilazimika kuogelea kwa takriban saa 11 hadi ufukweni mwa bahari.

”Ilikuwa mwendo wa saa tano usiku baada ya kumaliza kuvua ndani ya bahari hindi wakati boti yetu iliokuwa imetubeba ilipopinduka ghafla.Tulikuwa wavuvi sita na tukaanza kupeana moyo kwamba tuogelee polepole hadi ufukweni, lakini kwa ghafla kuna wimbi kubwa lilitupiga na kututawanya”.

Image caption

Matano ni mvuvi na muogeleaji wa kuwasaidia wavuvi

Matano ambaye ni mvuvi na muogeleaji wa kujitolea anasema kuwa baada ya ajali hiyo wenzake wanne waliangamia huku akisalia na mwenzake mmoja ambaye walisaidiana kuogelea hadi ufuoni.

Na tangu tukio la kisa hicho mvuvi huyo na wenzake wametilia mkazo swala la mawasiliano hatua iliowalazimu kuvumbua mbinu mpya ya kulinda usalama wao.

Nilipowatembelea wavuvi hawa katika ufukwe wa bahari wa Nyali mjini Mombasa mwendo wa saa kumi na mbili alfajiri, nilikutana nao wakiandaa nyavu zao pamoja na boti lao ili kuanza safari ya muda mrefu ndani ya bahari hindi.

Huwezi kusikiliza tena

Wavuvi watumia kondomu kulinda simu zao baharini pwani Kenya

Lakini kitu kilichonuvitia zaidi ni hatua yao ya kugawana mipira ya kondomu miongoni mwao!

”Sisi hutumia mipira hii ya kondomu ili kulinda simu zetu kutoingia maji wakati tunapokuwa baharini tukiendelea na shughuli zetu za uvuvi”, alisema mmoja ya wavuvi hao.

Image caption

Mvuvi akiajiandaa kwa safari ndefu ya uvuvi baharini wakati wa msimu wa kusi

Mvuvi huyo anasema kuwa wanapoingiza simu zao za mkononi katika mipira hiyo zinasalia kuwa salama na ni rahisi wao kuzungumza na wateja wao walio nchi kavu mbali na kuitisha msaada wakati wa hatari baharini.

Ni msimu wa kusi ambapo wavuvi hushauriwa na serikali kutofanya uvuvi kutokana na bahari iliochafuka na mawimbi makali.

Hatahivyo ufukara unawashinikiza wavuvi hao kuendelea na safari zao za uvuvi.

”Hatuwezi kuketi nyumbani kwa sababu ya tahadhari iliotolewa na serikali kwamba bahari ni chafu, sisi tuna familia zinazotutegemea, nani ataziangalia iwapo tutasalia nyumbani?”, Matano anauliza.

Katika jamii za kihafidhina kama hii inayoishi pwani ya Kenya, mipira ya kondomu hushirikishwa na tendo la ngono.

Haki miliki ya picha
Alamy

Hivyobasi ununuzi ama hata ubebaji wake ni swala linalozungumzwa kwa siri kubwa kutokana na kazi yake.

Kwa wengi ni mwiko kuonekana na kinga hiyo , hatua inayoweza kuwashangaza wengi unapopatikana ukitembea na mipira ya kondomu ambayo hazijatumika mfukoni.

Kulingana na wavuvi hawa swala la wao kuelekea nyumbani wakiwa wamebeba paketi za mipira hiyo limekuwa la kawaida.

”Kwa sasa wake zetu wamezoea kwamba wakati mwingi sisi hutumia mipira hii kuzuia simu zetu za mkononi kuingia maji tunapokuwa baharini. Lakini kitambo ilikuwa vigumu kuelezea unapokamatwa na mipira hii ambayo mara nyingi husahaulika katika mifuko lakini tulikuwa tukiwaelezea kwa umakini hadi wanaelewa”. alisema mvuvi huyo.

Huku harakati za kutaka kujipatia kipato kwa wavuvi hawa masikini zikiendelea , wasiwasi wao sio tu kiwango cha samaki wanachovua mwisho wa siku lakini kuendelea kufanya uvumbuzi utakaowahakikishia usalama waoSource link

Jenerali Davis Mwamunyange ateuliwa kwenye tume ya kuchunguza ghasia za baada ya uchaguzi Zimbabwe


Mkuu wa majeshi mstaafu wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange

Haki miliki ya picha
JWTZ

Image caption

Mkuu wa majeshi mstaafu wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange

Mkuu wa majeshi mstaafu wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange ameteuliwa na Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kuwa mjumbe wa tume ya watu saba itakayochunguza vurugu za baada ya uchaguzi nchini humo.

Rais mstaafu wa Afrika Kusini Bw Kgalema Motlanthe ataongoza tume hiyo inatarajiwa kumaliza kazi yake ndani ya miezi mitatu.

Tume hiyo inatarajiwa kuchunguza kiini cha vurugu hizo ambazo zilipelekea vifo vya watu sita baada ya wanajeshi kuzima maandammano ya wapinzani siku mbili baada ya uchaguzi wa Julai 30.

Uchaguzi huo ambao umehalalisha urais wa Mngangagwa ulitazamiwa kuwa ni mwanzo mpya wa siasa za kidemokrasia tangu kung’olewa madarakani kwa Robert Mugabe Novemba 2017. Hatahivyo, kuingia kwa jeshi mtaani na kuwafyatulia risasi waandamanani kumezua mashaka juu ya mustakabali wa Zimbabwe.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Watu 6 waliuawa baada ya maafisa wa usalama kufyetua risasa dhidi ya waandamanaji wa upinzani

Swali kuu zaidi ni kuwa wengi wametaka kujua nani hasa aliwaamuru wanajeshi kuzuia maandamano.

Jenerali Mwamunyange ambaye alikuwa mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa miaka 10 toka 2007 mpaka alipostaafu 2017 ndio mtu pekee katika tume hiyo mwenye usuli wa mambo ya kijeshi.

Mwanasheria kutoka Uingereza Rodney Dixon ambaye aliiwakilisha serikali ya Kenya katika kesi ya vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 katika mahakama ya ICC, The Heague ni moja ya wajumbe wa tume hiyo.

Wavuvi wanaotumia mipira ya kondomu baharini

Mjumbe mwengine kutoka nje ya Zimbabwe ni katibu mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Madola Chifu Emeka Anyaoku kutoka Nigeria.

Kutoka ndani ya Zimbabwe wajumbe ni Profesa Charity Manyeruke na Profesa Lovemore Madhuku kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe pamoja na Vimbai Nyemba ambaye ni rais wa zamani wa chama cha wanasheria wa Zimbabwe.Source link

Polisi mzungu afungwa miaka 15 jela kwa kumuua kijana mweusi


Roy Oliver in court

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Ni nadra sana polisi kuhukumiwa kifungo kwa kuua. Mawakili wake Oliver wanasema watakata rufaa.

Afisa wa polisi amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kwa kumpiga risasi na kumuua kijana mweusi huko Texas Marekani.

Roy Oliver, ambaye ni mzungu alifyatua risiia kw akw agari mabali likikuw lkikotoka kuwa kw akaramu moja huko Dallas mwezi Aprili 2017 na kumiu Jordna Edwars aliyekuw ana umir wa maiaka 15.

Ni nadra sana polisi kuhukumiwa kifungo kwa kuua. Mawakili wake Oliver wanasema watakata rufaa.

Familia ya Jordan inasema kifungo hicho ni kifupi sana.

“Atakuwa huru baada ya miaka 15 na hicho si cha kutosha wa sababu Jordan hatapata maisha tena,” mama wa kambo Charmaine Edwards, alisema.

Kipi kilitokea siku ya mauaji?

Usiku wa tarehe 29 Aprili 2017 polisi waliitikia ripoti za watoto waliokuwa pombe kwenye karamu moja huko Balch Springs.

Haki miliki ya picha
Mesquite Independent School District

Image caption

Marafiki wa Jordan walimtaja kama mtoto mwenye furaha ambaye alipenda kutabasamu

Polisi walikuwa ndani ya nyumba walipojaribu kumpata mwenye nyumba wakati walisikia kile waliamini kuwa ni sauti za risasi, hali iliyozua hofu nyumbani na kusababisha watu kukimbia.

Kulingana na nyaraka za polisi, mwenzeke, polisi mwingine Tyler Gross alijaribu kusimamisha gari lililokuwa limejaa ambao walikuwa wakiondoka kwenye karamu.

Alitembea kwenda kwa mlango wa abiria wa gari na kugonga kioo, ambacho kilivunjika.

Oliver kisha akafyatua risasi mara kadhaa kwenda kwa gari, akampiga Jordan ambaye alikuwa amekataa mbele ya kiti cha abiria, nyumba ya kichwa.

Oliver alisema aliamini kuwa gari hilo lilikuwa linarudi nyuma kwenda kwa polisi mwenzake.

Hata hiyvo kamera ya polisi huyo ilionyesha kuwa gari hilo lilikuwa likiondoka kwa polisi wakati risasi hizo zilifyatuliwa.

Oliver alifutwa na polisi muda mfupi tu baada ya mauaji hayo.

Watu wanahisi vipi kuhusu hukumu hiyo?

Jaji huko Texas alimpata Oliver na hatia siku ya Jumanne na Jumatano akahukumiwa miaka 15 jela

Hii inamaanisha kuwa anaweza kupewa msamaha baada ya miaka saba unusu.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Familia ya Jordan iliangua kilio na kuwakumbatia waendesha mashtaka baada ya kusomwa hukumu.

Waendesha mashtaka walikuwa wanataka ahukumiwe kifungo cha miaka 60.

Familia ya Jordan iliangua kilio na kuwakumbatia waendesha mashtaka baada ya kusomwa hukumu.

Baba yake, Odell Edwaerds alisema alikuwa mwenye furaha sana.

Hata hivyo mama wake wa kambo alisema alitakiwa kifungo kirefu cha miaka 25 hadi 30.

Wakili wa familia ya Edwards Daryl Washington, alisema hukumu hiyo ni ishara kuwa kila mwamerika mweusi aliyeuawa na polisi hakupata haki.Source link