Kwa Picha: Kenya Airways yaanza safari za moja kwa moja hadi Marekani


Maafisa wa kipeperusha bendera za Kenya na Marekani kabla ya ndege aina ya Boeing 787-Dreamliner kuanza safari JumapiliHaki miliki ya picha
AFP/Getty Images

Image caption

Maafisa wa kipeperusha bendera za Kenya na Marekani kabla ya ndege aina ya Boeing 787-Dreamliner kuanza safari Jumapili

Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, limeanzisha safari za ndege za moja kwa moja kati ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na uwanja wa ndege wa Kimataifa wa JFK jijini New York.

Rais Uhuru Kenyatta Jumapili usiku aliongoza hatua hiyo ya kihistoria kwa sekta ya safari za ndege nchini Kenya alipozindua safari ya ndege ya kwanza, KQ Boeing 787-8 Dreamliner.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 234. Tiketi za kawaida zinauzwa Sh89,000 ($890).

Ndege hiyo itachukua muda wa masaa 15, hii ikiwa imepunguza muda wa zamani wa safari hiyo kwa masaa saba.

Ndege hiyo iliondoka JKIA saa tano kasorobo usiku na inatarajiwa kuwasili uwanja wa JFK saa kumi na dakika 25 alasiri.

Safari ya kwenda Marekani itapunguzwa kwa saa sabaHaki miliki ya picha
AFP/Getty Images

Image caption

Safari ya kwenda Marekani itapunguzwa kwa saa saba

Miongoni mwa abiria waliosafiri kwa ndege hiyo katika safari yake ya kwanza ya moja kwa moja kutoka Nairobi hadi jijini New York ni Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni balozi Monica Juma na balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec.

Rais Kenyatta alimkabidhi Balozi Juma bendera ya Kenya huku afisa mmoja wa Ubalozi wa Marekani akimkabidhi balozi Godec bendera ya Marekani.

Kenyatta na RutoHaki miliki ya picha
UHURU KENYATTA/FACEBOOK

Abiria wengine katika ndege hiyo ni Katibu wa Wizara ya Uchukuzi Esther Koimett na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Kenya Airways Sebastian Mikosz.

Rais Kenyatta na William RutoHaki miliki ya picha
UHURU KENYATTA/Facebook

Uzinduzi wa safari hiyo ya kwanza ya Ndege kwenda jijini New York, ni hatua kubwa kwa sekta ya uchukuzi wa ndege nchini Kenya hasa kwa kuimarisha sekta mbali mbali za kiuchumi kama vile utalii na biashara.

DreamlinerHaki miliki ya picha
UHURU KENYATTA/FACEBOOK

Safari za ndege za moja kwa moja hadi nchini Marekani, zitaipa fursa nchi ya Kenya kunufaika na uchumi wa marekani, ambao ndio mkubwa zaidi ulimwenguni na vile vile katika eneo zima la kaskazini Marekani.

Mambo muhimu kuhusu safari hiyo:

  • Safari hiyo itachukua saa 15 kutoka New York hadi Nairobi na saa 14 kutoka Nairobi hadi New York.
  • Shirika hilo limesema litatumia marubani wanne na wahudumu 12 wa ndege.
  • Safari yote itatumia tani 85 za mafuta.
  • Shirika hilo litatumia ndege zake za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner ambazo huwabeba abiria 234.
  • Ndege za kwenda Marekani zitaondoka JKIA Nairobi saa 23:25 na kufika JFK kesho yake saa 06:25.
  • Ndege za kurudi Nairobi zitaondoka New York 12:25 na kutua JKIA saa 10:55 kesho yake.

Safari hii ina maana gani kwa Kenya?

Shirika la ndege la Kenya Airways linahudumia vituo 40 barani Afrika pekee mbali na safari zake za ndege katika bara Ulaya, Asia, Mashariki ya kati na maeneo ya bara hindi.

Uzinduzi wa safari hizo za ndege kunatarajiwa kuvutia mashirika mengi ya kibiashara kwa soko la Kenya na kuongezea kwa zaidi ya makampuni 40 ya Marekani ambayo yamefanya Jiji la Nairobi kuwa makao makuu kwa huduma zao barani Afrika.

Vile vile, safari hizo za ndege za moja kwa moja zitaongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini Kenya huku serikali ikikadiria kwamba safari hizo zitasaidia kuleta watalii wengi mashuhuri na wa kibiashara.

Maeneo ya Afrika ya mashariki na ya Kati pia yatanufaika kiuchumi kutokana na hatua hiyo ya hivi punde katika sekta ya safari za ndege nchini Kenya.

Kabla ya shirika la ndege la Kenya Airways kupewa kibali cha ndege zake kusafiri moja kwa moja hadi jijini New York, Halmashauri ya Usimamizi wa Safari za Ndege nchini (KCAA) ilihitajika kutimiza masharti ya Halmashauri ya Ukadiriaji wa Safari za Ndege za Kimataifa ambayo yanatolewa na Shirika la usimamizi wa safari za Ndege nchini Marekani na hivyo kupewa kibali cha safari zake mwaka jana wa 2017.

Mbali na Kenya, mataifa mengine ya Afrika yanayoendesha safari za moja kwa moja hadi Marekani ni, Cape Verde, Misri, Ethiopia, Nigeria na Afrika Kusini.

Picha zote zina hakimilikiSource link

Zanzibar: Tunguja na vijiwe vidogo vinavyotumika kufundishia madrasa na kuwafanya wanafunzi kuzingatia masomo yao


wanafunzi

Kusini mwa Zanzibar nchini Tanzania, kuna utaratibu usio wa kawaida ambapo baadhi ya wanafunzi wa madrasa wamekuwa wanawekewa vijiwe vidogo au hata tunguja (nyanya pori) kwa lengo la kuwafanya wanafunzi hao kuzingatia masomo yao.

Mwalimu Jecha Sule Mohamod kutoka chuo cha madrasatul-Qadiriya kisiwani Zanzibar, anasema mbinu hizo zilikuwa zinatumika tangu zamani ukiwa ni ubunifu wa kuwafanya watoto watulie na kuzingatia kile wanachofundishwa.

Jecha anaeleza kwamba zamani kulikuwa na njia mbalimbali za kufundishia kama vile kusoma kwa kutumia mbao na wino maalumu ili kuwafundisha watoto namna ya kuandika lugha ya kiarabu na kuhifadhi kile walichofundishwa.

“Tulikuwa tunafundishwa jinsi ya kuzingatia kile ambacho tunafundishwa kwa kuwekewa kijiwe chini ya kidevu hivyo mwanafunzi akishawekewa tu anakuwa anaangalia pale ambapo anafundishwa,” anasema.

“Njia hii pia inasaidia kwa sababu madrassa zetu ziko mtaani karibu na barabara ambapo watu wanapitamara kwa mara hivyo mwalimu kuwadhibiti wanafunzi inakuwa ngumu inabidi amuwekee kijiwe ili ashughulikie masomo yake badala ya kuangalia mambo mengine.”

Huwezi kusikiliza tena

Tunguja zinatumika kuwafanya wanafunzi kuzingatia masomo yao

Hata hivyo wanaamini kuwa njia hiyo ni ubunifu unaoangalia mazingira husika yakoje na wanaamini kuwa utamaduni huo umeweza kuleta matokeo chanya ya upatikanaji wa viongozi wa dini kama vile mashehe na maimamu.

Wanaamini pia ili kufikia mikakati mizuri ya taaluma lazima ubunifu uhusike.

Kwa nini watoto hawa wanaweza kuzingatia masomo kwa njia hii

Wanafunzi wanakuwa wanaelewa na sio tu kuimba bila kuelewa.

Image caption

Tunguja inatumika kufundishia

Mwalimu Haji Mohamed Mahamud anasema kwamba lengo la mbinu hii ni kumfanya mwanafunzi kutoshughulika na kitu chochote zaidi ya kusoma.

Mtoto akiangusha tunguja hiyo huwa anaonywa tu lakini sio kuadhibiwa.

Ukimuona mtoto ana michezo mingi unamuwekea ili aweze kuzingatia katika kusoma.

Muda wa kukaa nayo inategemea na lazima apate mazoezi kujua kuweka tunguja hiyo, kama hana mazoezi hawezi kukaa nayo hata dakika moja.

Mbinu ambayo wanaitumia ni kuweka kitu kimoja kinachoitwa tunguja unamuwekea chini ya kidevu na kuinamisha uso .

Huwezi kusikiliza tena

Kisiwani Zanzibar, madrassa zatumia nyenzo za asili kufundishia

Hapo anaweza kushughulikia kusoma na lazima apate mazoezi kabla lakini hapo badae hatawekewa tena.

Kwa upande wao wanafunzi, wanaona njia hiyo ni nzuri na inawasaidia kuzingatia masomo na moja ya mazoezi kwao.

Mohamed Simba ,mkazi wa Makunduchi ni mwanaharakati anayekubaliana na matumizi ya njia hizi za ufundishaji.

Simba anaamini kuwa walimu huwa wana saikolojia ya kutosha ya kujua kama watoto wamechoka basi wanapaswa kutafutiwa njia mbadala.

“Ni vizuri kuchukua maoni ya walimu wa madrassa kwa kuwa wao ndio wanajua mazingira halisi wanayoyafanyia kazi na wanajua wanafunzi wanaowafundisha.

Hivyo kama wanaofundisha vyuo vya madrassa wakiona kwamba kutumia njia hizi za kutumia tunguja,

vijiwe au nyanya pori ili kuwafanya wanafunzi kuzingatia katika masomo ni vyema kwa sababu hata sisi tulitumia njia kama hizo” Simba alisema.

Kusoma na kuweza kufahamu na kuzingatia, kuna kusoma kwa aina nyingi kuna kusoma kwa kuimba lakini pia kuna kusoma kwa kuzingatia.

Hata hivyo njia hiyo ni mila ambayo imekuwepo ingawa sasa imeanza kutoweka baada ya baadhhi ya watu kulalamikia kuwa ni unyanyasaji kwa watoto.Source link

Lipstiki upakayo inaweza kukuletea maradhi ya sarataniBidhaa za lipstiki

Image caption

Wataalamu wanashauri kuto nunua bidhaa zinazo kuwa katika maduka yasiyo rasmi yaani vibanda

Kila uchao baadhi ya wanawake hupakaa rangi za mdomo maarufu kama lipstiki ikiwa ni sehemu ya kuendea urembo na umaridadi wa mwili.

Aina hii ya vipodozi inayopakwa kwenye ngozi ya nje ya mdomo inakuja katika sampuli na rangi tofauti japo maarufu zaidi ni zile za rangi nekundu, na zipo ambazo hung’arisha mdomo bila kuwa na rangi yeyote.

Kuna ambazo huvumilia maji yaani water proof kwa lugha ya kingereza. Zipo za maji, za mafuta na kavu. Baadhi hutoka kila unapokula nyingine hudumu mpaka kwa saa 24.

Gharama za bidhaa hizo hutofautiana na mahali mteja amenunua na pia ubora. Nchini Tanzania, zipo lipstiki za bei nafuu mpaka kuanzia Sh500 ambazo hizi hupatikana mitaani na minadani. Lakini pia zipo za bei ya juu mpaka Sh50,000 na zaidi, ambazo huuzwa kwenye maduka makubwa na hutangazwa kuwa ni halisia.

Haki miliki ya picha
Plaxeder&Magreth

Image caption

Kuna kila aina ya Lipstiki, zipo za maji,kavu na za mafuta.

Changamoto kubwa katika bidhaa hizo ni ubora na usalama, kwani zipo ambazo huaminika wazi wazi kuwa si salama yaani sio halisia na ndio hupatikana kwa bei rahisi zaidi. Lakini zile za bei ya juu zaidi hutangazwa kutoka uingereza ndio yasemekana ni halisi zaidi.

Watumiaji wengi wameiambia BBC kuwa bei ndio huwa kigezo kikuu wanachoangalia ili kubaini ubora wa urembo huo.

Lakini je bei ndio kipimo pekee cha ubora?

BBC imezungumza na Gaudensia Simwanza ambaye ni meneja mahusiano na elimu kwa umma kutoka mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) juu ya usalama wa bidhaa hizi za urembo wa mdomo ambazo mara nyingi huingia kinywani hasa wakati wa kula au kunywa.

“Bidhaa lazima isajiliwe, kupitia usajili ndo tunaamini kua mtu anaweza tumia bila kupata madhara, kwasababi kuna vitu tunaangalia katika usajili mfano uhalali wa bidhaa, taarifa zilizo wekwa je ni sahihi, iliko toka je imesajiliwa? Pia tunaang alia ubora wa bidhaa yenyewe na vifungashio vyake kwa sababu tuna viwango vyetu. Viungo vilivyo wekwa kwenye bidhaa vimewekwa kwenye lebo na je viungo hivyo ni salama? Kuna wengine husema bidhaa imetoka kwenye kiwanda hiki kumbe kiwanda hicho hakipo. Baada ya hapo lazima bidhaa tupeleke maabara kwaajili ya vipimo.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hata hivyo ameongeza kuwa zipo baadhi ya bidhaa zina viambata ambavyo haviruhusiwi nchini Tanzania hivyo huzuiliwa. Bi Gaudensia pia ametoa rai kwa watumiaji wa urembo huo kununua bidhaa kwenye maduka yanayoeleweka.

“Tunaangalia sifa za kikemikali na kibaiolojia, katika viambato tunaangalia kama vilivyo tumika ni salama kwa sababu kuna baadhi ya viambato ambavyo havitakiwi kama vile steroid, mercury compound, hydroquinone na vinginevyo. Na bidhaa ambazo tumezisajili unazikuta zipo kwenye tovuti yetu, lakini kikubwakwa mtu wa kawaida tunamwambia nunua kwenye maduka ambayo yana tambulika, kwa sababu unanunua kwenye maduka rasmi inakusaidia hata ukipata tatizo unarudi hapo tofauti na hkununua mtaani au zilizo wekwa chini kesto ukija huta mkuta,” Gaudensia anaiambia BBC

Mwaka 2007 ilifanyika tafiti kupitia kampeni ya vipodozi salama huko Marekani iliyo itwa “A poison Kiss” yaani busu lenye sumu. Utafiti huo uligundua kemikali ya lead kwenye asilimia 61 ya lipstick 33 zilizo fanyiwa utafiti.

Wataalamu wa dawa wanasema hakuna kiwango cha kemikali ya lead ambacho ni salama kwenye damu.

Mwanafunzi aliyejilipia karo kwa kumtengenezea Lil Wayne mkufu

Hata hivyo utafiti huo unasema hakuna lipstiki ambayo imeorodhesha kemikali ya lead kuwa sehemu ya kiungo chake. Kiwango chake ni kidogo lakini uwepo wa kemikali hiyo katika lipstiki ama shedo ambayo hupakwa na kunyonywa kupitia ngozi inaleta wasiwasi wa usalama wa bidhaa za urembo ambazo hutumiwa na wanawake wengi duniani.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hata hivyo katika utafiti uliofanywa na mamlaka ya chakula huko marekani, waligundua kemikali ya ulead katika lipstiki au shedo zote 400 walizo zifanyia utafiti. Kiwango chake kilikuwa kikubwa maranne zaidi ya utafiti wa kampeni ya vipodozi salama.

Lakini pia utafiti wa Chuo kikuu cha Calfonia wao walichunguza lipstiki nane na lipshine 24 na walikuta chemikali zingine ambazo ni sumu kama vile chromium, cadmium, manganese, aluminum na hiyo lead.

Kemikali ya Lead inamadhara gani?

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, kemikali ya lead ina sumu ambayo huathiri mifumo mingi ya mwili wa binadamu. Na zaidi ni sumu kwa watoto. Kemikali hiyo katika mwili wa binadamu husambaa katika ubongo, ini, figo na mifupa. Inatunzwa katika meno na mifupa ambapo hujiongeza kwa muda.

Katika wakati wa mimba sumu hiyo ya kemikali ya lead huenda moja kwa moja kwnye damu na humuathiri mtoto na hakuna kiwango cha kemikali hiyo kinachotajwa kuwa ni salama.

Watafiti wanasema kemikali hiyo huathiri kwa baadhi kupata mzio yaani hu washwa midomo. Madhara mengine ni kuzuia vitundu vya hewa kwenye mwili. Na baadhi ya viungo huleta hatari ya kupata saratani.

BBC imezungumza na Daktari wa Saratani Heri Tungaraza kutoka Hospitali ya Taifa muhimbili anasema kama lipstiki hiyo ina kemikali ya lead basi hatari ya uwezekano wa kupata saratani upo japo kua hakuna tafiti inayoelekeza ni kiasi kipi cha kemikali hiyo ambacho ni salama.

Haki miliki ya picha
Babieprecious

Image caption

Baadhi ya hizi bidhaa kama ukitumia ambayo si salama zinakufanya unapendeza kwa muda, lakini baadae huleta madhara.

“Zipo bidhaa ambazo zina kemikali hiyo na ambazo hazina. Kemikali ya lead imekuwa ikihusishwa sana na saratani ya figo, tumbo na mgongo. Kwa hiyo uhusiano upo lakini hakuna tafiti iliyo fanyika ikaangalia kiasi cha kemikali hiyo iliyopo kwenye lipstiki na kusema moja kwa moja inaleta saratani ya aina gani. Hivyo kama kweli lipstiki imebeba kemikali hiyo basi ni vyema mtumiaji akahoji kabla ya kutumia. Pia watu waache kununua vitu mitaani wanunue bidhaa ambazo zimesajiliwa na zinatambulika vyema zilipo toka, Tungaraza anaiambia BBC

Nae Daktari Romana Malikusema kutoka SANITAS hospitali anasema kweli kuna madhara kuanzia kwenye madhara ya kawaida kama mzio mpaka yale madhara makali kama kuingiza kemikali sumu katika mwili endapo mtu atatulia lipstiki isiyo salama.

“Inategemea na bidhaa imetengenezwa kwa kemikali zipi, baadhi ya hizi bidhaa kama ukitumia ambayo si salama zinakufanya unapendeza kwa muda huo lakini baadae huleta madhara, ni kama vile watu wanavyo jipaka foundation mara nyingi huzeeka haraka inaondoa ule uhalisia inatoa kabisa uhalisia wa ngozi hivyo hata hali ya ngozi kusinyaa inakuja haraka,” Dokta Romana anaiambia BBC

Hata hivyo Daktari huyo ameshauri kuwa watu wawe makini na bidhaa za urembo, wasome lebo na kujua ukomo wa kila bidhaa. Pia amesisitiza kuwa ni bora kununua ya gharama ambayo ni bora kuliko ya bei rahisi ambayo huenda ni si salama.Source link

Utamaduni wa kipekee wa mahari Rwanda: Mwanamke kulipa pesa kwa mwanaume ili aolewe


wanawake

Katika kijiji cha Nyamashekhe kilichopo mkoa wa magharibi nchini Rwanda kumekithiri utamaduni wa wanawake kulipa pesa kwa mwanaume ili waolewe.

Mtindo huo mpya wa maisha umezua gumzo katika jamii huku baadhi ya watu wakihoji hatima ya siku zijazo za utamaduni wa kulipa mahari.

BBC imetembelea kijiji hicho na kuzungumza na wanawake, wanaume, viongozi wa kijiji na baadhi ya wahusika ili kufahamu zaidi kwa nini utamaduni huo unazidi kupata umaarufu.

Kaitesi Lilian mmoja wa kina mama wa kijiji hicho anasema “Mvulana anapokuja kumposa msichana wako unajua kwamba mambo yameiva, lakini ndoa ikikaribia unaskia kwamba amemgeuka na kumwambia kwamba ndoa haitawezekana ikiwa hatapewa pesa za mahari”.

Alipoulizawa mbona wanawake wengine wameolewa bila kufuata utaratibu huo alifafanua kwa kusema”Wakati huo binti alikuja na kuangua kilio huku akinishinikiza niuze kila kitu hata mabati au shamba ilimradi yeye apate pesa ya kumpa mchumba wake.

Tofauti na maeneo mengine ya nchi ambapo mwanaume ndio hutoa posa kwa familia ya mwanamke, utamaduni huu mpya unawashinikiza wasichana kumlipa pesa mwanamume.

Inasadikiwa kuwa pesa hizo ni kama dola 1500 na huongezeka kulingana na uwezo wa familia ya msichana.

Waliyoshuhudia wanasema pesa hizo lazima zipatikane kwa udi na uvumba.

Lakini ni nini kinacho wafanya vijana kugeuza utamaduni uliopo?

Katika tamaduni za wanyarwanda mahari lazima itolewe tena na bwana harusi mtarajiwa.

Hata kama mahari haijakamilika kwa wakati huo familia husika zinakubaliana jinsi itakavylipwa, na hatimae harusi hufanyika.

Katika mkoa wa msgharibu nchini Rwanda pesa hizo zikikosekana hakuna harusi tena.

Kaibanda Bernard ameiambia BBC kuwa vijana “Wanafanya hivyo wakisema idadi ya wasichana sasa hivi ni kubwa sana”

Wasichana wengine wameshindwa kuvumilia, ambapo msichana akitinga umri wa miaka kumi na tano hivi anatafuta pesa kwa nguvu ili aweze kumnunua bwana.

Vijana wenyewe wanaona ni ishara ya ushirikiano katika familia mpya kutokana na hali ya maisha ilivyo ghali siku hizi.

John Gatera anasema mmoja wa watu wanaounga mkono mtindo huo wa maisha anasema “Zamani kutoa mahari ilikuwa ni kitu rahisi sana ni ngombe labda na kiwanja lakini sasa hata kupalilia sehemu ya ujenzi lazima ulipe pesa”.

Anasema yeye binafsi akifikisha umri wa kuoa lazima msichana amlipe pesa la sivyo harusi haitafanyika.

Baadhi ya watu katika kijiji cha Nyamashekhe wanataka serikali kuingilia kati suala hilo.

Mmoja wao ni mzee Kaihura ambaye anasema”Kijana hawezi kupata heshima katika jamii ikiwa hatatoa mahari”.

Utamaduni huu mpya umepokelewaje?

  • Wazazi waliyo na mabinti waliyofikisha umri wa kuolewa wana wasisi huenda mtido huo mpya wa maisha ukaenea kote nchini ikiwa hatua hazitachukuliwa kuukomesha
  • Pia wanahofia suala hili huenda likabadilisha kabisha utamaduni wa jadi wa wanaume kulipa mahari.
  • Vijana hususana katika mkoa huo wanadaiwa kujiona ”mastaa” hali ambayo huenda ikawafanya kuzembea majukumu yao ya familia hata wakifanikiwa kupata mwake zao.

Sio mara ya kwanza Mkoa huo wa Magharibi ambao ndio mkubwa kuliko mikoa mingine kuzua gumzo kuhusiana na masuala ya kijamii.

Kabla ya mtindo huu wa sasa wa vijana kutaka walipwe pesa na wasichana ili wawaoe, kulikuwa na wakati inadaiwa kuwa mvulana akimtembelea mchumba wake kwao sharti achinjiwe jogoo.Source link

Mbwa Mwitu waliopakwa rangi Zimbabwe


Mbwa mwitu hawa wenye muonekano wa kupendeza wanaitwa mbwa mwitu waliopakwa rangi.

Haki miliki ya picha
©Nicholas Dyer

  • Je ni mbwa kama mbwa wengine?

Haki miliki ya picha
©Nicholas Dyer

‘Lycaon pictus’ ni jina lao la kisayansi, ambalo linamaanisha kitu kama “rangi ya mbwa mwitu”.

Wana sauti yenye kupendeza inaweza kusafiri hadi kilomita 2 na wana masikio yao makubwa yaliosimama.

Haki miliki ya picha
©Nicholas Dyer

Wana sifa ya kuwa wawindaji wenye ufanisi zaidi barani Afrika kwa asilimia 80 na wanaweza kuwa kiwango cha juu zaidi kuliko ya simba au chui.

Haki miliki ya picha
©Nicholas Dyer

Haki miliki ya picha
©Nicholas Dyer

Haki miliki ya picha
©Nicholas DyerSource link

Sababu ya wanawake kuwa na nguvu ndogo, kuliko unavyodhania


WanawakeHaki miliki ya picha
Wanawake

Image caption

Getty Images

Utafiti ambao umetolewa kuwa, wanaume wengi wanashikilia nyadhifa kubwa kubwa kuwaliko wanawake, umewashangaa wengi. Kile ambacho hakikutarajiwa ni kwamba, kila mara wanawake wanashinikiza kuwepo na usawa.

Mataifa mengi mara nyingine hujaribu kujitokeza katika juhudi zao za kuwapa nyadhifa kubwa kubwa kina dada.

Kwa mfano, Rwanda ambayo iliwapa wanawake nusu ya vyeo katika baraza lake la Mawaziri. Hatua hiyo ilitokea siku chache tu baada ya usawa wa kijinsia kushuhudiwa katika baraza la Mawaziri nchini Ethiopia.

Kwingineko, duniani kuna mifano chungu nzima ya wanawake kuwa sawa na wanaume na hata mara nyingine kufanya kazi nzuri mno kuwaliko wanaume, kuwa na nguvu na hata maarufu.

Ingia mahakamani nchini Slovenia na utawakuta majaji wa kike kuwa mara nne zaidi ya mahakimu wa kiume. Katika taaluma ya uanhabari, Namibia imebobea: nusu ya vyeo katika vyumba vya habari vinashikiliwa na wanawake.

Sio vigumu kupata mataifa mengine, ambayo inakwenda sambamba na wala hili hasa kwenye kazi na taluma fulani. Nusu ya watalamu wa mitambo yaani IT nchini Malaysia ni wanawake, sambamba na kila wanaume 10 utawakuta 6 ni wanawake katika taluma ya utafiti wa matibabu nchini New Zealand na wanawake 5 kati ya watu 10 nchini Oman ni wanawake.

Wanawake wanaoshikilia nyadhifa katika kazi ambazo mara nyingi hufanywa na wanaume, wanazidi kuongezeka.

Na bado hata kama inaonekana ni swala la kawaida, mataifa mengine yanafa kupata mafunzo kutokana na mifano hii, huku kila mmoja akijiuliza je! umaarufu uko wapi?

Nguvu ya majaji

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Ruth Bader Ginsburg ni mmojawepo wa majaji watatu wa kike katika mahakama ya juu zaidi nchini Marekani

Jipya katika mawazo ya watu wengi, ni utata unaomzunguka Jaji wa Mahakama kuu nchini Maekani Bw Brett Kavanaugh, licha ya kuwepo kwa madai ya kuwabughudhi wanawake kimapenzi, swala ambalo amelikanusha kwa kinywa kipana. Mahakama kuu hiyo ambayo, majaji 3 kati ya 9 ni wanawake- ni mfano wa mfumo ambayo majaji wakuu, wanashikilia nguvu nyingi sana.

Nchini Uingereza, mfumo wa kisheria, imo chini ya sheria za kawaida. Majaji mara nyingi wanateuliwa mwisho katika taluma yao- mara nyingi kupitia mitandao iliyosheheni wanaume- na sheria zinategemea uamuzi wao na busara zao.

Fauka ya hayo, katika mataifa mengine kama vile Ufaransa na Slovenia, nguvu za majaji zimefinywa mno. Katika mifumo ya sheria ya kiraia- ambayo ni msingi wa sheria iliyoandikwa – majaji utumia busara zao ili kufanya tafsiri zao wenyewe za sheria na hukumu.

Wakufunzi wa sheria huwa majaji kwa kupita mtihani enye ushindani mkubwa, ili kuingia moja kwa moja kwenye mafunzo, mara baada ya kufuzu.

Vyeo hupewa kutokana na limu ya mtu huku cheo huongezwa mabegani ili kuleta tofauti kubwa.

◾Wanawake ambao wanaota kugawana mamlaka

◾BBC wanawake 100 mashuhuri mwaka 2018: Ni nani yuko kwenye orodha hiyo?

◾Mhadhiri mwanamke mweusi pekee katika historia nchini Uingereza

◾Kwa nini nusu ya waamerika huingiwa na wasiwasi, wakati ambapo mwanamke huyo anaugua

Majaji 6 kati ya 10 nchini Ufaransa ni wanawake, lakini cheo hicho huja na kupotea kwa malipo. Mara nyingi mawakili wanaofanya kazi za kibinafsi hupata mishara minono kuwaliko wale walioajiriwa na erikali.

Asilimia kubwa ya majaji wa kike wamo katika jamii ya baada ya utawala wa Kisovieti. Kwa mfano Slovenia. Majaji 7 kati ya 10 nchini Romania na Latvia ni wanawake.

Chini ya utawala wa ukomunisti, ukumu la Jaji sio tu kupata malipo duni, lakini pia walipitia mambo ya kiitikadi- mamlaka kuu ilikuwa kwengine. Hadi asa idara ya mahakama katika mataifa hayo, ina sifa duni na majaji wangali wakipata mihahara midogo.

Baada ya mageuzi

Katika talum nyingine, mara nyingi hali ni kwamba wanawake wanazidi kupata nguvu, hasa kufuatia kipindi cha mageuzi.

Ka mfano, katika sera za ukomunisti nchini Bulgaria, Uandishi habari ulikuwa chini ya serikali. Lkaini baada ya mwaka 1989, uhuriu wa habari ulikuwa kwa kasi na wanawake wengi waliokuwa wamesoma na wajasiriamali, walibadilisha mikondo ya taaluma zao na kujiunga na vyumba vya habari, na idadi yao kupanda na kuwa sawa na wanaume.

Nchini Rwanda swala la usawa wa kijinsia Bungeni lilianzishwa mwaka 2003. Hatua hiyo ilitoka baada ya kuharibiwa kwa taasisi za serikali wakati wa mauwaji ya halaiki, yalitokea nchini humo maka 1994.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Rais wa Rwandan Paul Kagame na wabunge wapya 80 mwezi Septemba, 2018

Wabunge 6 kati ya 10 nchini Rwanda ni wanawake, hatua inayoiweka nchi hiyo ndogoi ya Afrika kuwa katika nafasi ya kwanza kote duniani.

Lakini huko pia, kuna maswali chungu nzima kuhusiana na ni nani anayeshilia mamlaka kuba zaidi ya ytaifa.

Kiongozi mkuu mwanamume nchini Rwanda Bw Paul Kagame, ameshutumiwa kwa kuongoza taifa kwa mkono wa chuma. Wengi wamehoji kuwa, kuwepo kwa wabunge wengi wa kike, haikutoi fursa yoyote ya kugawana mamlaka.Source link

Kwa miaka 40 fuvu la Mangi Meli kutoka Tanzania limekuwa likitafutwa nchini Ujerumani


Mnyaka Sururu MboroHaki miliki ya picha
Tahir Della

Image caption

Mnyaka Sururu Mboro aliamuahidi nyanya yake kuwa angeleta nyumbani vuvu la Mangi Meli

Shinikizo linazidi kuongezeka nchini Ujerumani na Uingereza kuzitaka nchi hizo kurejesha mafuvu yaliyotolewa Afrika kwa utafiti zaidi ya karne moja iliyopita.

Raia wa Tanzania anayeishi nchini Ujerumani Mnyaka Sururu Mboro, amekuwa akitafuta fuvu lililotoweka la Mangi Meli kwa miaka 40.

Mangi Meli, chifu kutoka eneo la kaskazini ya sasa ya Tanzania aliuawa mwaka 1900 kwa kupambana dhidi ya utawala wa ukoloni wa Ujerumani.

Baada ya kuuawa mwili wake uliakatwakatwa na kichwa chake kikasafirishwa kwenda nchini Ujerumani.

Lilipo fuvu lake bado haijulikani, lakini baada ya wakfu unaofahamika kama Prussian Cultural Heritage wa mjini Berlin kugundua mafuvu zaidi kutoka Tanzania, imempa Bw Mboro matumaini mengi.

Haki miliki ya picha
National Museums in Berlin

Image caption

fuvu

Anatoka eneo sawa na alilokuwa akitoka Mangi Meli, na mwaka 1977, kabla hajaondoka kwenda kusoma Ujerumani alimuambia bibi yake kuwa angetafua fuvu hilo.

Watafiti wamegundua mabaki 200 kutoka Tanzania mengi yakiwa ni mafuvu ambayo yalichukuliwa wakati nchi bado ilikuwa chini ya utawala wa Ujerumani.

Tangu Oktoba mwaka 2017 wamekuwa wakichunguza ilikotoka mifupa iliyo kwenye hifadhi yao ambayo inatajwa sasa kuwa maelfu.

Mradi wao ulianza mwaka mmoja baada ya mwandishi wa habari raia wa Ujerumani kufichua kiwango cha mabaki kutoka nchi zilizokuwa makoloni ya Ujerumani.

Watafiti pia wametambua mafuvu 900 kutoka Rwanda na takriban kati ya 400-500 kutoka Togo na Cameroon – hizi ni nchi zilizokuwa sehemu ya makoloni ya Ujerumani kati ya mwaka 1884 na 1918.

Haki miliki ya picha
National Museums in Berlin

Image caption

Mwanasayansi Felix von Luschan alitoa wito kwa mavuvu kupelekwa Ujerumani

Maziko mazuri yatakiwa

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga amesema serikali inataka kujadili kurejeshwa mabaki hayo.

Maziko mazuri ndicho kilicho akilini mwa Bw Mboro.

Anasema kuwa ikiwa atarejesha fuvu la Mangi Meli kwenda Moshi kaskania mwa Tanzania atapata amani kwa kuwa mwili chifu huyo uliokatwa unahitaji kukamilika.

Bw Mboro ambaye sasa anaishia mjini Berlin anatoka jamii sawa na ile ya Chifu Meeli aliyeuawa na alikuwa akiambiwa hadithi za ujasiri wake.

Nyanya yake alimwambia jinsi alibaki muasi hadi siku ya kifo chake.

Mangi Meli alinyongwa pamoja na watu wengine 18 lakini alichukua muda wa saa saba kufa ishara ya jinsi alikuwa jasiri, Bw Mboro alisema.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Mwezi Agosti wanawake wa Herero walihudhuria misa mjini Berlin ambapo mavuvu ya Namibia yalirejeshwa

Bw Mboro alikuwa ametumia miongo minne kushinikiza mamlaka kufungua makavazi na kuangalia mabaki hayo ya binadamu.

Kwanza ilikuwa ni kupuuza kuliko kakataa ndiyo ilizuia kutafutwa, anasema.

“Kila mtu niliyekuwa nikimuuliza alisema hakufahamu chote kuhusu historia.”

Lakini baadaye aligundua kuwa makavazi ya Charité mjini Berlin yalikuwa na mafuvu na mwaka na 2000 wataalamu wawili waliruhusiwa kuyatazama.

Waligundua kuwa kulikuwa na takriban mafuvu 70 kutoka Tanzania, lakini kulingana na rekodi hakukuwa na vuvu la Mangi Meli.

Image caption

Zilizokuwa koloni na Ujerumani Afrika

Kwa Bw Mboro matumaini ni kuwa vuvu la Mangi Meli litarejeshwa, anaendea kusubiri licha ya serikali yake kuonyesha nia ya kurudisha mabaki ya watu.

Lakini Bw Mboro anahisi ni hali nyingine kuchelewa tena na anahofu huenda asitimize ahadi alitoa kwa bibi yake.Source link

Adam Zakaria Kinyekire: Mtanzania aliyetengeneza helikopta aunda gereji la kuhama hama linalohudumu hadi Zambia


Adam Kinyekire aliwahi kuunda helikopta lakini ikapigwa marufuku

Image caption

Adam Kinyekire aliwahi kuunda helikopta lakini ikapigwa marufuku

Adam Zakaria Kinyekire anajulikana zaidi kwa jina la ‘Street Engineer’, na yeye ni fundi mekanika kutoka Wilaya ya Tunduma, mkoa wa songwe, nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Alijifunza kazi hiyo mwenyewe bila kuhudhuria chuo chochote, lakini ni maarufu kwa kuunda helikopta na pia huwafaa madereva kwa gereji lake la kuhama hama.

Adam anasema yeye ni mbunifu ambaye hakupata ujuzi wowote kutoka shuleni maana mara baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida na baadaye akaanza kuunda vitu kama vile mashine ya kusagia nafaka, gari la karakana na hata helikopta.

“Ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali huwa sifundishwi na mtu ni kitu tu ambacho kipo kwenye damu, ni kama vile ndoto tu ambapo vitu vinakuja kwenye akili kwamba naweza kutengeneza hiki na hiki lakini sijawahi kupata mafunzo popote,” Adam Zakaria anaeleza.

Kwa sasa anafanya kazi na vijana takribani 40 na wengine zaidi ya 500 walipita katika mikono yake kupata mafunzo.

Kwa nini Adam aliamua kutengeneza gereji linaloweza kusafiri?

Sababu iliyompelekea kutengeneza gari la aina hiyo ni baada ya kubaini kwamba kuna wakati watu wanakosa huduma wakiwa mbali ndio maana akaamua kutengeneza mashine ambayo inatembea.

“Watu wengi huwa wanaharibikiwa na magari yao katika maeneo ambayo hakuna msaada.”

Gari hili lina vitendea kazi vyote vya ufundi, mfumo wa umeme na huduma ya kwanza yaani kila kitu kinachopatikana kwenye garage kipo katika gari hili.

Wateja wangu wengi ni Watanzania ambao wana magari makubwa ya mizigo yanayoelekea au yanayotoka Zambia.

Zambia ina pori kubwa hivyo wakikwama inawawia vigumu kutengeneza.

“Kila siku magari yanakatika hivyo unaweza kukuta naenda mara mbili kwa wiki au mara nne kwa mwezi ila lazima niende”, Adam aeleza.

Gari hili ambalo hulitumia kama gereji la kuhama hama, alilitengeneza kwa muda wa mwaka mmoja na sasa liko barabarani ni miaka saba, na anasema gari hilo lina manufaa makubwa sana sio kwake tu bali hata vijana ambao wanafanya nao kazi.

“Hii mashine inajitengeneza yenyewe na tunaweza kulipa ada za watoto shuleni,” anasema Adam.

Image caption

Adam amewasaidia vijana wengi kwa ajira

Hata hivyo bado anakabiliwa na changamoto ya kibali cha gari hilo ingawa anashukuru kuwa nchini Zambia huwa hawamsumbui kwa sababu limeunganishwa na gari jingine lenye namba ya usajili.

Gari linasafiri mpaka kilomita 600 kwenda kufuata magari yaliyoharibika nchini Zambia, mteja hulipa gharama ya huduma yake kulingana na kazi na eneo.

Na huwa anafuata utaratibu wote wa kujaza vibali ili kuingia nchi ya pili kufanya kazi yake.

“Ubunifu wangu unatokana na fikra zangu”.

“Niliwaza kuanzisha gereji la namna hii baada ya siku moja kunusurika na ajali baada ya kukutana na gari barabarani limeziba njia,”Adam alisimulia.

Licha ya gari hili Street Engineer amejifunza kutengeneza vifaa vingine.

Wanaonufaika na huduma

Magari kuharibika njiani ni dharura na ni kawaida kwa binadamu, huwa inatokea kwa bahati mbaya hata kama madereva wamejiandaa.

Issa Hamza Abdala ni dereva wa magari makubwa, na anasema kuwa aliwahi kumuita fundi huyo mara mbili wakati lake gari lilipokatika chesesi.

“Licha ya kuwa huwa tunatembea na vifaa vyetu lakini gari likikatika inabidi uombe msaada.

“Mafundi wa Zambia na Watanzania ni tofauti, magari mengi sana huwa yanamtumia.

“Kuna wakati nilimkuta hata Matumbo huko, zaidi ya kilomita 15 kutoka Tunduma .

“Ni rahisi kwetu kumtumia fundi ambaye tunamfahamu, ila ubora wa kazi yake pia ndio sababu kubwa ya kuamini kazi yake”, alisisitiza dereva.

Ernest Chikoti anashukuru kwa uwepo kwa huduma hii ya Adam.

“Namba yake kaisambaza na ana vifaa vyote basi unaweza kumpigia simu na kumtumia picha katika whatsapp aone tatizo lililokupata na inakuwa rahisi kumpata na kututengenezea.

Image caption

Adam na gereji lake

Nilimfahamu Street Engineer kwa kuambiwa na watu kuwa kuna fundi ambaye alishawahi kutengeneza helikopta ndio anaweza kutengeneza magari vizuri.

Huyu mtu ameamua kubuni yeye kama yeye lakini ni vyema kwa serikali kuwawezesha wengine wabuni vitu kama hivi licha ya kuwa huyu hakuwezeshwa lakini tunahitaji huduma hii zaidi,” Ernest alisisitiza.

Kutengeneza helikopta

Adam Kinyekire ni miongoni mwa Watanzania ambao wamo kwenye historia ya kutengeneza ndege aina ya helikopta.

Adam aliiambia BBC kuwa alifanikiwa kutengeneza ndege hata kabla ya kuiona ndege aina hiyo katika maisha yake yote.

Ilimchukua kipindi cha miezi sita mpaka mwaka kuikamilisha ndege hiyo.

Lakini ndoto yake iliishia patupu baada ya serikali kumpiga marufuku.

Wataalam wa masuala ya anga, wanasema kuwa kuna utaratibu katika kila jambo na wabunifu wanapaswa kutambua kanuni na sheria zilizopo.

“Wazo hilo lilinijia baada ya kuona nimetengeneza gereji linalotembea na kuona kuna umuhimu wa kuanza kupambanua akili kwa kubuni jambo jingine ambalo lingeweza kuwa na manufaa kwangu,” Adam anasema.

Hata hivyo shauku yake hiyo ya kuona ndege ikiruka katika runinga ilimpa hamasa ya kutengeneza ndege iweze kuruka kama nyingine zinavyoruka.

“Nilianza kwa kuangalia ni kitu gani kinachosababisha ndege iruke na kubaini kuwa ni nguvu ya upepo ambayo ikitengenezwa itakuwa na uwezo wa kuinua ndege.

Huwezi kusikiliza tena

Adam Kinyakile: Mwenye gereji ya magari inayowafuata wateja Tanzania

Ndege yangu nimeitengeneza kwa vifaa vya magari na mpaka sasa inaweza kuruka lakini utaalamu wa kuifanya itue bado.

Ingawa nilipata hofu sana baada ya tangazo la gazeti kutoka likitoa onyo kwa watengenezaji wa ndege na nilikata tamaa pia lakini sasa nina nguvu ya kuanzisha vitu vingine pia,” Adam aeleza.

Pamoja na jitihada nyingi ambazo amezitumia kutengeneza ndege hiyo ambayo haikuwa na manufaa, Adam anashukuru kwamba chuo cha sayansi na teknolojia kiliona jitihada zake na kumuwezesha kwenda kuona ndege kwa macho yake na kumpa mafunzo ya kutengeneza mashine ambazo zitanufaisha jamii na yeye mwenyewe.

Picha zote: Eagan Salla, BBCSource link

Wanawake 100 wa BBC: Mke wa Albert Einstein alikuwa mtu wa aina gani?


Mileva Einstein alikuwa mwanafizikia mwenye kipaji adimu kivyake lakini waandishi wa vitabu kuhusu maisha yake wanaamini alizuiwa kung’aa na mumewe Albert Einstein.

Ingawa walifanya kazi kwa pamoja na alitoa mchango mkubwa, hilo halikutambuliwa na hajapewa heshima anayostahiki.Source link